Pages

Thursday, February 3, 2022

WAZIRI NCHEMBA APOKEA UGENI WA BENKI YA DUNIA KATIKA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akijiandaa kumpokea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Corporation), Bw. Makhtar Sop Diop, wakati akishuka kwenye ndege alipowasili Uwanja wa Ndege, jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Corporation-IFC), Bw. Makhtar Sop Diop, alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja katikaUwanja wa Ndege jijini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiwa na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Corporation) nchini, Bw. Makhtar Sop Diop, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege jijini Dodoma akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini.



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Corporation) nchini, Bw. Makhtar Sop Diop (kushoto), mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

…………………………………………………………………

Na Eva Valerian na Saidina Msangi, WFM-Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la kimataifa-IFC, Bw. Makhtar Diop amewasili jijini Dodoma akitokea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo anatajia kukutana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kujadili namna shirika hilo linavyoweza kusaidia maendeleoya Sekta binafsi hapa nchini

Bw. Diop amepokelewa leo asubuhi katika Uweanja wa Ndege wa Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na baadae kuelekea Ikulu ya Chamwino.

Akizungumza kwa kifupi akiwa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Bw. Diop amesema kuwa lengo la ziara yake ni kujadili na Uongozi wa nchi namna ya kuiwezesha sekta binafsi nchini Tanzania kukua na ili iweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Baadae, Dkt. Mwigulu na Mgeni wake waliekea Ikulu ya Chamwino-Dodoma kukutana na Mheshimiwa Rais Samia Sukluhu Hassan, kwa ajili ya mazungumzo na leo mchana Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia katika Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Makhtar Diop atafanya mkutano na wadau wa sekta binafsi na kuhitimisha ziara yake kwa kuzungumza na vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment