Mkurugenzi
Mtendaji, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Wakili, Bi. Anna Henga
(katikati) akizinduwa rasmi Ripoti ya Haki za Binadamu na biashara
nchini ya mwaka 2020/21 jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Wakili, Bi. Anna Henga
(wa nne kulia) pamoja na wageni waalikwa, wafanyakazi wa kitengo cha
utafiti LHRC wakionesha nakala ya ripoti hiyo mara baada ya kuizinduwa
rasmi jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Wakili, Bi. Anna Henga
(wa nne kulia) pamoja na wageni waalikwa, wafanyakazi wa kitengo cha
utafiti LHRC wakionesha nakala ya ripoti hiyo mara baada ya kuizinduwa
rasmi jana jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezinduwa Ripoti ya Haki za
Binadamu na biashara nchini ya mwaka 2020/21 huku kikibainisha uwepo wa
changamoto mbalimbali na kutolea mapendekezo ili kuleta maboresho
endelevu ya sekta hiyo.
Akizinduwa
ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji, Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu. Bi. Anna Henga (Wakili) alisema ripoti hiyo
ni matokeo ya utafiti uliofanywa na LHRC kwa mikoa 15 ya Tanzania Bara,
ikihusisha kutembelea maeneo ya kazi na biashara kwa kampuni /mashirika,
wanajamii, mamlaka ya udhibiti, na maafisa wa serikali za mitaa.
Wakili
Bi. Henga amesema ripoti imeangazia pia haki za binadamu na uchunguzi
juu ya maswala yanayohusu biashara na haki za binadamu huku akibainisha
vyanzo vya data za ripoti kupatikana kupitia njia anuai zikiwemo vyombo
vya habari, kukagua ripoti, sheria, sera, kanuni na hati zingine juu ya
sheria za kazi, haki na viwango vinavyotengenezwa na wahusika wa ndani
na wa kimataifa.
Aidha
alisema ripoti ya 2020/21 imeangazia hali ya haki za Binadamu na
biashara ikiwa ni pamoja na hali ya athari za UVIKO-19 katika sekta ya
biashara hususani kwenye mikataba ya ajira kati ya wafanyakazi na
waajiri, usitishwaji wa ajira usio haki na ulipwaji wa mishahara. Ripoti
hiyo pia imeangazia suala la hifadhi za jamii na changamoto zinazohusu
wafanyakazi katika michango ya mifuko hiyo ya hifadhi za jamii.
"...Kwa
kipekee ripoti imezungumzia haki za wafanyikazi madereva wa mabasi na
malori ambao wanakabiliwa na masuala mengi ikiwa ni pamoja na kufanya
kazi kupita kiasi, malipo kidogo, ukosefu wa kandarasi zilizoandikwa au
nakala za mikataba, haki ya kuunda na kujiunga na vyama vya wafanyikazi,
ukosefu wa mikataba na usalama wa kazi. Utafiti wa ripoti hii umegundua
masuala anuwai katika mchakato wa ununuzi wa ardhi kwa madhumuni ya
uwekezaji, uwajibikaji wa kijamii na kuheshimu haki za binadamu pamoja
na matukio ya uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuliza viwanda,".
Wakili
Bi. Henga ameongeza kuwa tafiti imebaini Mikataba ya ajira imeshuka
ambapo wafanyakazi wengi walioshiriki katika utafiti asilimia 59
walisema wana mikataba ya ajira, huku asilimia 41 wakisema hawana
mikataba, ilhali Idadi yawafanyakazi wenye mikataba ya ajira ni pungufu
ya asilimia 25 ukilinganisha na idadi ya wafanyakazi wenye mikataba hiyo
katika utafiti uliopita wa mwaka 2019, ambapo asilimia 84 walidai kuwa
na mikataba ya ajira.
"
Ndugu wageni waalikwa; Utafiti huu pia ulibaini obwe kubwa la
kukosekana kwa uelewa juu ya sheria za kazi na ajira baina ya
wafanyakazi, na hii imepelekea wafanyakazi wengi kutokujua ni wakati
gani haki zao zimekuwa zikivunjwa. Mkoa wa Tabora uliongoza kwa kuwa na
asilimia kubwa zaidi ya wafanyakazi wasio na uelewa wa kutosha kuhusu
sheria na kanuni za kazi (92%). Mikoa mingine ni pamoja na Mbeya (83%),
Shinyanga (82%), Mara (81%), Tanga (78%), Dodoma (76%), Singida (73%),
Mtwara (72%), na Manyara (71%).
Alizitaja
haki za wafanyakazi zilizoripotiwa kukiukwa zaidi kwa ripoti ya mwaka
2020/21 ni; Kutolipwa mishahara, Kucheleweshwa kwa malipo ya mshahara,
usitishwaji wa ajira kwa njia isiyo ya haki, punguzo la mshahara lisilo
na haki, vitisho vya maneno, udhalilishaji wa maneno, kukataliwa kwa
likizo/ kupunguzwa kwa siku za likizo, kufanya kazi saa nyingi bila
kupumzika (zaidi ya kawaida na muda wa ziada wa kazi), wafanyakazi
kukataliwa kuwa na mikataba/nakala za mikataba hiyo, kutolipwa kwa muda
wa ziada, mazingira yasiyo salama ya kazi na pia kukosekana kwa
utaratibu wa fidia pale mfanyakazi anapoumia akiwa kazini.
"...tungependa
kuiasa serikali kupitia na kuboresha au kubadilisha viwango vya
mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kwani Waraka wa Serikali
kuhusu Viwango vya Mishahara unaotumika ni wa mwaka 2013. Hata hivyo,
waraka huo unatakiwa kupitiwa kila baada ya miaka 3 ili kuboresha
mishahara na masharti ya kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa. Kuna haja ya
kufanyia mapitio waraka huu na kuona namna ya kuboresha mishahara ya
wafanyakazi wa kada mbalimbali ili kuwasadia kukidhi gharama za maisha
huku tukitambua haki ya kuishi maisha ya hadhi kama mojawapo ya haki
muhimu ya binadamu," alisema Wakili Bi. Henga.
Alisema
ripoti hiyo itasambazwa maeneo mbalimbali na kuwataka wadau wote
kuisoma na kufanyia kazi mapendekezo kwa ajili ya kuimarisha hali ya
haki za binadamu na biashara nchini, na pia kuifanya iwe chachu ya
mabadiliko ya hali ya uchumi unaozingatia haki za binadamu nchini.
No comments:
Post a Comment