Pages

Friday, July 30, 2021

KATIBU MKUU KIONGOZI ZANZIBAR ATOA PONGEZI KWA GLOBAL EDUCATION LINK

Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata maelelezo kutoka kwa maofisa wa wakala mkubwa wa kuunganisha wanafunzi na vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea jijini Dar es Salam.


 Maafisa wa Global Education Link  wakitoa  maelelezo kwa wananchi walio fika kwenye banda hilo namna ya  kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali  vya nje ya nchi  leo katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoa wa Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV   

Maafisa  wa Wakala Mkubwa wa kuunganisha wanafunzi na vyuo vikuu nje ya nchi, Global Education Link wakiendelea na kazi ya kuwahundumia wanachi waliofika katika mbada hilo leo katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mkoa wa Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)

 Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zena Mohamed Said amepongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wakala wa Elimu Nje ya Nchi

Global Education Link (GEL) katika sekta ya elimu nchini kwa kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania na vyuo vikuu nje ya nchi.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea mabanda ya GEL yaliyopo katika Maonesho ya 16 ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo vyuo vikuu mbalimbali vimeshiriki.

Aidha katika maonyesho hayo GEL imefanikiwa kuleta vyuo vikuu 10 ambavyo ni washirika wake nje ya nchi kwa ajili ya kuja kuelezea fani wanazotoa.Vyuo hivyo ni Chandigarh, Lovely Professional University (LPU), CT, Maharish Makandeshwar, Pandeet Deendayal Energy, Sharda, Rayat Bahra vya India na VN Karazan na Sum State vya Ukraine.

Katibu Mkuu Kiongozi amesema "Ni kweli kutokana na uhaba wa fani mbalimbali wanafunzi wa hapa nchini wanalazimika kwenda nje ya nchi kusoma elimu ya juu, hivyo kuwa na kiunganishi kama GEL ni jambo la msingi katika kurahisisha upatikanaji wa vyuo hivyo.

"Ni kweli vyuo vyetu haviwezi kuchukua wanafunzi wote sasa nawapongeza nyinyi kwa kazi hii ya kuwaunganisha wanafunzi wetu na vyuo vya nje na pia kwa wale ambao wako tayari kushirikina na sisi,Serikali inawashukuru kwa mchango wenu,"amesema.

Awali Mkurugenzi wa GEL Abdulmalick Mollel amemueleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na vyuo hivyo kuwapeleka wanafunzi wa Tanzania kwa kozi mbalimbali ikiwemo mpango wa kubadilishana wanafunzi.

Ameongeza wakati Mollel nchi mbalimbali duniani zina kozi nyingi sana za afya kwa Tanzania bado hazijawa za kutosha, hivyo wanafunzi wanaotaka kozi hizo wamekuwa wakiwaunganisha kwenda kusoma kwenye nchi hizo.

Amesema wamezungumza na vyuo vingi vya nje ya nchi kuwa Tanzania kuna  wanafunzi wengi na wamekubali kuwachukua kwa gharama za hapa hapa ndani ."Wakati sisi tunajipanga kuongeza kozi za afya hapa nchini."

Mollel amesema baadhi ya vyuo vimeahidi kufungua matawi hapa nchini baada ya kuona mahitaji makubwa ya kozi wanazofundisha ambazo wanafunzi wa Tanzania wamekuwa wakizifuata kwenye mataifa yao.

Amesisitiza baadhi ya vyuo hivyo vya nje vitaingia makubaliano na vyuo vya hapa nchini kuhusu namna ya kufanyakazi pamoja katika utoaji wa elimu ya juu."Ujio wa vyuo hivyo ni fursa kwa vyuo vya Tanzania kuangalia namna ya kushirikiana kwenye kozi mbalimbali pamoja na kubadilishana wanafunzi wanaoendelea na masomo ili kupeana uzoefu.

Amefafanua kuwa mwanafunzi anaweza kusoma miaka miwili India na kisha akaja kumalizia hapa nchini Tanzania"Na wa hapa  anaweza kusoma mwaka mmoja na kisha akaenda kumalizia kwenye chuo cha nje, haya ni mambo ambayo vyuo vinapaswa kuangalia namna ya kushirikiana."

No comments:

Post a Comment