Pages

Friday, July 30, 2021

Tanzania yaishukuru GIZ ya Ujerumani kwa kampeni ya usafi

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akionyesha baadhi ya sabuni na zana za usafi za Emina zinazotengenezwa na BINGWA Laboratories zikatazotumika katika kampeni ya usafi jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya usafi iliyofanyika eneo la Feri kwa ufadhili wa Shirika la Ujerumani GIZ na kuendeshwa na asasi ya Emmanuel Brotherhood Foundation (EBF).
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akinawa mikono kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya usafi jijini Dar es Salaam inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ na kampeni hiyo kufanywa na Emmanuel Brotherhood Foundation (EBF) katika wilaya tano za Dar es Salaam.
Baadhi ya wauza samaki, baba na mama lishe wa soko la Ferry jijini Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya usafi mkoani humo iliyofadhiliwa na serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Maendeleo GIZ na mradi kuendeshwa na Emmanuel Brotherhood Foundation (EBF).
Mmoja wa mama lishe aliyehudhuria uzinduzi wa kampeni ya usafi akionyesha bidhaa za usafi za Emina zinazotengenezwa na BINGWA Laboratorie zitakazotumika kwenye kampeni hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam usafi itakayoendeshwa na asasi ya Emmanuel Brotherhood Foundation (EBF) na inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika lake la GIZ chini ya mradi wake wa DeveloPPP. Kampeni hiyo ya usafi itahusisha mama na baba lishe, makondakta na madereva wa daladala ambapo imelenga kuwafikia watu 25,000 Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Tanzania imeishukuru serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la Maendeleo la GIZ chini mradi wake wa DeveloPPP kwa kudhamini kampeni ya kutoa elimu kuzuia magonjwa ya kuambukiza na kutoa bidhaa mbalimbali za usafi bure kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Meya wa Jiji Omar Kumbilamoto wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi itakayoendeshwa na taasisi ya Emmanuel Brotherhood Foundation (EBF) kwenye Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema walengwa kwenye kampeni hiyo ya usafi ambayo itahusisha viongozi wa serikali za mitaa ni mama na baba lishe, wauzaji wa samaki, madereva wa daladala na makondakta waMkoa wa Dar es Salaam ambapo wanufaika wanatarajiwa kuwa 25,000.

“Tunawashukuru sana GIZ na EBF kwa kutoa vifaa vya usafi niwahakikishie kwamba mmeleta sehemu sahihi lakini naomba msiishie hapa Dar es Salaam nendeni mikoani nako mkafanya kampeni kama hii na mtoe sabuni za usafi kama mlivyofanya hapa,” alisema Meya

Amesema Jiji la Dar es Salaam halijapata milipuko ya magonjwa kwa muda mrefu kutokana na kampeni mbalimbali za kuweka mazingira katika hali ya usafi hivyo kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka kufanya usafi kuwa ajenda endelevu.

Mshauri wa EBF Alex Benson alisema kupitia mradi huo vifaa vya usafi vitakavyotolewa bure ni pamoja na ndoo na sabuni za kunawa mikono, dawa za kuua vijidudu, vitakasa mikono na taulo za kike zitawasaidia walengwa kufanyakazi katika mazingira safi.

Amesema nia ya mradi huo ni kuhakikisha mazingira yao ya biashara yanakuwa safi kutokana na ukweli kwamba magonjwa ya kuambukiza yanaweza kuzuilika kwa njia ya usafi na watu watu wakiwa na afya njema wanashiriki vizuri shughuli za uchumi.

Amesema takwimu za miaka ya hivi karibuni zinaonyesha kuwa serikali imekuwa ikitumia takriban asilimia 70 ya bajeti ya afya kugharamia matibabu ya magonjwa ya kuambukiza yanayosababishwa na uchafu wa mazingira.

Ameongeza wadau wa mradi huo watatoa elimu na kuhamasisha utamaduni wa usafi katika jamii ili kulinda afya ya jamii kwa ujumla kwani magonjwa mengi yanazuilika kwa njia ya usafi.

Aidha ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya kwa kuidhinisha matumizi ya vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali na kusaidia kuratibu kampeni hiyo ambayo itawanufaisha watanzania wengi.

“Kipekee tunaishukuru serikali ya Ujerumani kupitia shirika lake la GIZ kwa kuona umuhimu wa kufadhili kampeni hii ya usafi na kuyatumia makampuni ya ndani kama Bingwa Laboratories Ltd na AFRICRAFT kutengeneza bidhaa zinazotumika katika kampeni hii, kwa pamoja tunasema magonjwa mengi yanazuilika kwa njia yaa usafi.” Alisema

 

No comments:

Post a Comment