Na Said Mwishehe,Michuzi TV
CHUO cha Ualimu cha Mafunzo ya Ufundi Stadi Morogoro(MVTTC)kimewashauri
wanafunzi wanaosomea fani ya umeme kutembelea banda la chuo hicho lililopo kwenye jengo la VETA katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.Akizungumza leo, Mhandisi Frank Urio ambaye ni mwalimu wa umeme katika chuo hicho cha mkoani Morogoro amesema katika maonesho hayo wamekuja na kifaa cha kufundishia wanafunzi wanaochukua fani ya umeme, kufika kwenye banda hilo.
"Tunawaomba wanafunzi waje ,na wajitokeze kwa wingi ili waje kupata elimu stahiki kuhusu umeme na kama mnvyojua sisi ni chuo kwa hiyo tupo hapa hadi Julai 13 mwaka huu, tumedhamiria kujibu kila tutakachoulizwa kuhusi kozi tunazotoa chuoni kwetu ikiwemo hii ya umeme,"amesema Mhandisi Urio.
Aidha ametoa mwito kwa wanafunzi wanaosomea fani ya umeme kufika kwenye banda hilo kwa lengo la kufahamu kwa kina kuhusu umeme kupitia vifaa walivyonavyo kwenye maonesho hayo.
Kwa upande wake Mkufunzi Mwandamizi katika chuo hicho Sophia Tuka ametumia nafasi hiyo kuelezea kozi ambazo zinatolewa na chuo hicho zikiwemo kozi za ualimu na wanaandaa walimu wanaofundisha ufundi.
Pia kwenye chuo chao wanafundisha ualimu ngazi ya cheti na diploma na Septemba mwaka huu wanaanza muhula wa masomo ,hivyo ametoa rai kwa watanzania kwenda chuoni hapo kwa ajili ya kupata ujuzi.
No comments:
Post a Comment