Pages

Friday, July 2, 2021

MBUNIFU NA MGUNDUZI KUTOKA VETA ALIYEBUNI KIFAA CHA KUFUNDISHIA ELIMU YA SAYANSI YA ANGA AIPONGEZA SERIKALI, ATOA NENO



Na Said Mwishehe,Michuzi TV

ERNEST Malanya ambaye ni Mbunifu na Mvumbuzi kutoka Chuo cha Ufundi( VETA) Chang'ombe mkoani Dar es Salaam amevumbua kifaa ambacho kinatumika katika sayansi ya elimu ya sayansi ya sayari ya jua kitaanza kutumika kufundishia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Kwa mujibu wa Mbunifu huyo kutoka VETA ni kwamba wanafunzi watakuwa na fursa ya kujifunza somo la sayansi inayohusu sayansi ya sayari ya jua na hasa inavyofanya kazi.

Akifafanua zaidi akiwa kwenye Banda la VETA kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalim Nyerere maarufu Sabasaba , Malanya amesema wanafunzi wanauwezo wa kujifunza ana kwa ana na kuona sayari hiyo inavyoweza kulizunguka jua kwa njia ya vitendo na ubunifu huo umepita hatua mbalimbali ili kufanyiwa tathimini na Mamlaka zinazohusika na mfumo wa elimu ,pia kifaa hicho kimepita Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.

Amesisitiza "Ubunifu huu umepitishwa kupitia mitaala mbalimbakli ili kuweza kufundishia kwenye shule za msingi na sekondari na ni sehemu ya mapendekezo ambayo yalitolewa na Serikali ambapo ilinitaka kufanya hivyo. Serikali ilinitaka nipeleke miongozo ambayo itawezesha kufundishia darasani  na muongozo huo ni wa vitabu  ambao utakuwa unawaongoza walimu kuweza kufundishia wanafunzi.

"Kwa sasa  muongozo huu umekamilika na nimeshaukabidhi kwa mamlaka husika na kinachoendelea sasa ni kuchapisha vitabu vya kutosha ili kuweza kutumika,.amesema.na kuongeza ameshakabidhi vitabu hivyo na ripoti yake ya maboresho ya vitabu.Vitabu hivyo amekabidhi Mei mwaka huu na rai ameto ombi  kwa Mamlaka itoe idhini ili vianze kutumika.

 Malanya ameishukuru Serikali hadi alipofikia   na hatua iliyopo  kwa sasa ni kuona kitabu hicho kinavuka mipaka kwa wanafunzi kupata elimu stahiki ya elimu ya sayansi ya anga.Kifaa hicho kinakwenda kuondoa changamoto ya ufundishaji shuleni kuhusu elimu ya sayansi ya anga.

 

No comments:

Post a Comment