Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Tume ya Utumishi wa Umma)
Bw.Richard Cheyo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam
baada ya kuhitimisha mkutano wa nne wa mwaka wa Fedha 2020/2021.Pichani
kulia ni Katibu Msaidizi, Idara ya Rufaa na Malalamiko Peleleja Masesa
akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
kuhusiana na masuala mbalimbali ya TUME ya Utumishi wa Umma kupokea na
kutolea uamuzi rufaa 107 na malalamiko 8 yaliyowasilishwa na watumishi
wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na mamlaka zao za ajira
na mamlaka za nidhamu.
Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa kwenye mkutano huo
Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakielezwa kwenye mkutano huo
TUME ya Utumishi wa Umma imepokea na kutolea uamuzi rufaa 107 na malalamiko 8 yaliyowasilishwa na watumishi wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na mamlaka zao za ajira na mamlaka za nidhamu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Tume ya Utumishi wa Umma) Richard Cheyo baada ya kuhitimisha mkutano wa nne wa mwaka fedha 2020/2021.
Cheyo amesema Tume ilijadili na kutoa uamuzi wa rufaa 107, ambapo rufaa 76 zilikataliwa, rufaa 09 zilikubaliwa bila masharti na rufaa 12 zilikubaliwa kwa masharti kuwa mashauri hayo yaanzishwe upya kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
Aidha amesema kuwa rufaa 10 zilikatwa nje ya muda hivyo zilitupiliwa mbali na tume."Tume ilipokea na kutolea uamuzi malalamiko 08 kati ya hayo malalamiko 03 yalikataliwa. Malalamiko 05 yalikubaliwa bila masharti,"amesema Cheyo.
Amesema Tume katika kushughulikia na kutoa uamuzi wa rufaa na malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake, ilibaini kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria, kanuni, taratibu na miongoni mwa watumishi wa Umma, na baadhi ya waajiri, mamlaka za ajira na mMamlaka za Nidhamu.
Cheyo amesema Watumishi wa Umma,Waajiri, mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanapaswa wakati wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria,kanuni.Taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali.
Hata hivyo amesema kamati za Uchunguzi zinazoundwa na Mamlaka za Nidhamu kuchunguza tuhuma wanazokabiliwa nazo watumishi wa umma zinatakiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Amesema Waajiri wanatakiwa kushughulikia masuala ya kinidhamu ya watumishi wanaotuhumiwa kufanya makosa kwa wakati ili hatua stahiki zichukuliwe na ikithibitika kuwa hawana makosa wastaafu kwa heshima.
Amesisitiza kuwa Watumishi wote wa Umma wanapaswa kuzingatia Kanuni za Maadili katika Utumishi wao na kutoa huduma bora kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment