Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi
akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia
kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa
kutoka mikoa ya Shinyanga (Kiloleli – Kishapu) na Dar es salaam
(Mabwepande, Saranga, Kivule na Majohe) leo Jumatatu Juni 28,2021 katika
ukumbi wa TGNP Mabibo jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde -
Malunde 1 blog
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya
Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa
vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga na Dar es
salaam

Mwezeshaji
katika mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa
habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya
Shinyanga na Dar es salaam, Deogratius Temba akitoa mada kuhusu Bajeti
ya Mrengo wa Kijinsia.
Afisa
Habari wa TGNP, Monica John akizungumza wakati mafunzo ya Bajeti yenye
mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo vya
taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga na Dar es salaam
Washiriki
wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambao ni waandishi wa
habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya
Shinyanga na Dar es salaam wakiwa ukumbini.

Shinyanga na Dar es salaam wakipiga picha ya kumbukumbu.
Washiriki
wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambao ni waandishi wa
habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya
Shinyanga na Dar es salaam wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blo
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amepongeza
mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan akisema inazingatia masuala ya usawa wa kijinsia hali
itakayosababisha maendeleo yaende kwa haraka.
Liundi
ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 28,2021 akizungumzia Siku 100 za
uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mafunzo ya
Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa waandishi wa habari na viongozi wa
vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Shinyanga (Kiloleli –
Kishapu) na Dar es salaam (Mabwepande, Saranga, Kivule na Majohe)
yanayofanyika katika ukumbi wa TGNP Mabibo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
huyo wa TGNP amesema katika siku 100, serikali ya awamu ya sita
imeonesha mwelekeo mzuri katika kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia.
“Suala
la jinsia ni suala la maendeleo,ni suala la uchumi, ni suala la kila
kitu, hivyo ni lazima tutoe kipaumbele. Uchumi umekuwa ukiyumba kutokana
na masuala ya kijinsia kutopewa uzito. Tunatarajia kwa mwelekeo huu
tunaokwenda nao katika awamu ya sita pia hata maendeleo yatakwenda kwa
haraka”,amesema Liundi.
“Tumeona
masuala ya usawa wa kijinsia kwenye uongozi ,ni kitu ambacho
tumekizungumza kwa muda mrefu tangu mkutano wa Beijing na utekelezaji wa
azimio la Beijing, awamu zilizopita zilifanya juhudi zake lakini awamu
hii ya sita imekuja na juhudi ambazo ni tofauti, ambazo zinatusogeza
mbele zaidi.
Kwa
hiyo tukiona Kiongozi wa nchi anazungumza wazi wazi kwamba kwenye
masuala ya uongozi atatoa kipaumbele pia kwa wanawake wenye uwezo. Na
tumeona anachofanya, kwa upande wa Makatibu Tawala ameteua wanawake
asilimia 48, hii inakuwa ni kwa mara ya kwanza. Hiki ni kitu cha
kujivunia”,ameeleza Liundi.
“Hizi
siku 100 ni za kusherehekea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan amelipa
kipaumbele suala la usawa wa kijinsia. Tumeona pia majaji ameteua
wanawake asilimia 42.8, mabalozi asilimia 33.3 lakini pia wakuu wa
wilaya asilimia 31”,amesema Liundi.
Amesema
kutokana na hali hiyo hivi sasa kwamba mwendo uliopo ni wa tofauti,
mambo yanaenda vizuri kinachotakiwa ni kutoa ushirikiano, wale
waliochaguliwa na kuteuliwa waendelee kujitoa, wafanye kazi vizuri, kwa
uaminifu, uadilifu ili kuonesha kwa vitendo kuwa wanawake wana uwezo wa
ziada.
Aidha
amefafanua kuwa serikali ya awamu ya sita imeanza kuonesha mabadiliko
kwa kuangalia tunu za kuongoza taifa mfano masuala ya haki, kilimo
chenye tija, demokrasia, usawa na uhuru wa vyombo vya habari, kuondoa
umaskini na rushwa ikiwemo ubadhirifu wa mali za umma na ukusanyaji kodi
usio na bughudha.
Kuhusu
mageuzi ya kilimo ambapo mkulima mdogo, mwanamke ndiyo amebeba taifa
katika uhakika wa chakula , Liundi ameshauri mwanamke asije akatupwa
pembeni, kuwe na mikakati mahsusi ili kuhakikisha kuna ushiriki wa
wakulima wadogo wadogo hususani wanawake waliopo kwenye maeneo ya
pembezoni ambao wamekuwa wakiteseka kila siku huku akishauri wanawake
wapewe kipaumbele zaidi kwenye elimu ya ujuzi kwenye vyuo vya ufundi.
“Lakini
pia tumeona katika masuala ya madini,maji, elimu,afya uchumi, utalii,
viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano vinatiliwa uzito wa kipekee
kama vipaumbele vya maendeleo ya taifa, tunachotaka mwanamke asiachwe
nyuma na serikali imeshaonesha nia watu wote watanufaika”,amesema
Liundi.
Amesema
madhumuni ya mafunzo hayo kwa waandishi wa habari na viongozi wa vituo
vya taarifa na maarifa ni kuongeza na kuimarisha uelewa wa washiriki juu
ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa sababu suala la kijinsia ni
suala la maendeleo.
"Kwa
hiyo tunapokuwa na utengwaji wa rasilimali ambazo zinaangalia mtazamo
wa jinsia, makundi yote katika jamii yatafaidika na rasilimali za taifa
na ndiyo maana tunatia msisitizo”,amesema Liundi.
“Tunajua
kuwa Bajeti yetu ya taifa imepitishwa na Bajeti ikipitishwa tujue kuwa
mwaka mzima tutatembea katika huo mgawanyo wa bajeti. Hivyo kama
wananchi ni vizuri kufahamu ni kitu gani kimepita, vipaumbele gani
vimepitishwa hali itakayosaidia kufuatilia hizo rasilimali zinatumikaje
kwa kuzingatia makundi yote katika jamii”,ameeleza.
No comments:
Post a Comment