Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAHAKAMA kuu nchini Afrika Kusini imemuhukumu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo
Jacob Zuma kwenda jela miezi 15 baada ya kukutwa na hatia ya kutoshiriki vikao vya kamati maalum inayochunguza tuhuma zake za ufisadi na kujihusisha na rushwa alipokuwa madarakani.Hukumu hiyo imetolewa leo na jaji Khampepe Sisi ambaye amesema, hukumu hiyo haitakuwa ya lazima iwapo Jacob Zuma atazingatia na kuheshimu maagizo ya mahakama na kuanza kuhudhuria vikao vya kamati inayochunguza tuhuma za rushwa dhidi yake.
Awali Mwenyekiti wa kamati maalum inayochunguza tuhuma za Zuma, Raymond Zondo amekuwa akiiomba mahakama kumpeleke jela Zuma miaka miwili kwa kutoshiriki vikao vya kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment