Pages

Wednesday, March 31, 2021

WAZIRI NDALICHAKO AKABIDHI MAGARI 38 KWA WADHIBITI UBORA WA SHULE ZA KANDA NA WILAYA

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza na watumishi wa wizara hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Moshi Kabengwe,akieleze mikakati wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wakifatilia Hotuba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya Magari yaliyotolewa  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akikata utepe kuashiria ugawaji wa  Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiingia kwenye gari mara baada ya kukabidhi Magari 38  kwa wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiwa ndani ya gari akienda mara baada ya kuwakabidhi Magari 38  wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akimkabidhi ufunguo wa gari Mdhibiti Mkuu ubora wa Shule Kanda ya Ziwa Bw.Victor Bwindiki  mara baada ya kuwakabidhi  Magari 38  wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akiwa na Naibu wake Mhe Omary Kipanga wakimsikiliza Mdhibiti Mkuu ubora wa Shule Kanda ya Ziwa Bw.Victor Bwindiki wakati akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Kukabidhi Magari 38 kwa Wadhibiti Ubora wa Shule za Kanda na Wilaya hafla iliyofanyika leo Machi 31,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ,amekabidhi magari 38 kwa

wadhibiti ubora wa shule za Kanda na Wilaya huku akimuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Ubora nchini kumpelekea taarifa ya ukaguzi wa shule na walichokibaini katika ukaguzi huo.

Kauli hiyo ameitoa leo Machi 31,2021 jijini Dodoma wakati wa  hafla hiyo ya kukabidhi ya kukabidhi magari .Prof Ndalichako amesema kuwa anatoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi huyo kumpelekea ripoti ya tathmini ya shule hizo .

Waziri Ndalichako amesema kuwa haridhishwi na mfumo wa ukaguzi unaotumika kwa sasa ambao unasababisha matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma.

“Leo tupo hapa tunagawa magari haya kwa ajili ya wadhibiti ubora wa shule kuwawezesha kuzifikia shule kwa wingi na kwa wakati,lakini cha kushangaza mdhibiti ubora ataendesha gari kutumia mafuta ya serikali kwenda kata ambako kuna shule ya msingi na  sekondari lakini atakagua shule ya msingi na kuiacha sekondari,’’amesema Prof.Ndalichako

“Mkurugenzi nenda na wakati mimi nataka mkurugenzi anayeenda na wakati
kama huwezi tutatafuta wadhibiti ubora wa shule wanaokwenda na wakati
na wakati ili tuwe na matumizi mazuri ya rasilimali “amesema

Prof.Ndalichako ametumia  fursa hiyo kuwashukuru wahisani na wadau wa Maendeleo
wakiwemo Benki ya Dunia,SIDA pamoja na DfID ambao kupitia mrdi wa Lipa
kwa Matikeo (EP4R) wamewezesha ununuzi wa magari 38 kwa gharama ya
shilibgi bilioni 6.

“Magari haya yanagawiwa kwenye Halmashauri 27 zisizo na magari,kanda
10 na gari moja litatumika katika ofisi ya Makao Makuu ya Wizara kwa
ajili ya shughuli za ufuatiliaji.

Hata hivyo amesema kuwa Wizara yake kupitia Idara ya Udhibiti Ubora wa  shule
ina jukumu la kusimamia Mfumo wa Udhibiti Ubora wa shule na kufanya
tathimini ya ujifunzaji na ufundishaji katika shule na vyuo vya ualimu
na kutoa ushauri wa kitaalam na kitaaluma kwa walimu ,wakufunzi na
viongozi wa Elimu ili kuinua Ubora wa Elimu nchini.

Awali akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizar ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia ,Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Moshi Kabengwe
amesema kuwa magari hayo yamegawiwa kwa wadhibiti Ubora wa wilaya,Kanda na
Halmashauri zenye upungufu wa magari na ambazo magari yake yamechakaa
ambayo matengenezo yake yanahitaji fedha nyingi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary
Kipanga amewataka wadhibiti Ubora wa shule kuyatumia magari hayo kwa
malengo yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.

 

No comments:

Post a Comment