………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika Baraza la
Mawaziri na Mteua ...Katibu Mkuu Kiongozi Mpya.
Rais Mhe.Samia amefanya
mabadiliko hayo leo Machi 31,2021 Ikulu Chamwino Dodoma wakati wa hafla
ndogo ya kumuapisha Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.
Katika uteuzi huo, Rais Samia
Suluhu Hassan amemteua Balozi wa Tanzania nchini Japan, Hussein Yahya
Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally
ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.
Kwa upande wa mabadiliko ya
Baraza la Mawaziri, Rais Samia Suluhu Hassan amemhamisha aliyekuwa
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy
Mwalimu kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Seleman Jaffo
akipelekwa kushika nafasi ya Ummy Mwalimu.
Mwigulu Nchemba amepelekwa
wizara ya Fedha na Mipango akisaidiwa na Hamad Masauni na nafasi yake
katika Wizara ya Katiba na Sheria kuchukuliwa na aliyekuwa waziri wa
mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba
Kabudi akisaidiwa na Jofrey Mizengo Pinda.
Balozi Liberata Mulamula
ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika
Mashariki, huku naibu wake akiteuliwa Mbarouk Nassoro Mbarouk.
Kwa upande wa Wizara ya Nchi
ofisi ya Rais, utumishi na Utawala bora, ameteuliwa Mohamed Omary
Mchengelwa, huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Capt. George Mkuchika
akipangiwa kazi nyingine.
Wizara ya Uwekezaji imerejeshwa
katika ofisi ya Waziri Mkuu na kutolewa ofisi ya Rais, huku Godrey
Mwambe akiteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo na Prof. Kitila Mkumbo
akipelekwa wizara ya Viwanda na Biashara.
Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa wizara ya
Michezo, Sanaa, Utamaduni na Michezo, huku aliyekuwa naibu waziri wa
wizara hiyo, Abdallah Ulega akipelekwa wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa
naibu waziri.
Naye, Mwanaidi Ally Hamis ameteuliwa kuwa naibu waziri wa
pili katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto.
Akitangaza mabadiliko hayo, Rais
Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuondoka kwa Dk. Philip Mpango katika
Wizara ya Fedha na Mipango kumempa nafasi ya kulitazama baraza lote la
mawaziri na kufanya mabadiliko kidogo.
“Nimeona niwabadilishe kwa sababu tangu mumeapa ni
muda mfupi kuona nani ameshindwa, tunaanza na hawa awamu ya sita, jinsi
tunavyokwenda tutaona nani tunakwenda nae na nani tunamuacha.
“Naibu mawaziri mkatumike vizuri, kuna kudharauliana, naibu
anadharau waziri na waziri nae anadharau naibu, kazi ni kazi sitaki
kusikia kingine,” amesisitiza.
Katika upande mwingine, Rais
Samia amefanya uteuzi wa wabunge watatu ambao ni Dk. Bashiru Ally,
Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk
No comments:
Post a Comment