Pages

Thursday, December 31, 2020

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU AKABIDHI ZAWADI KWA WASIOONA

 Msaidizi wa Makamu wa Rais Maendeleo ya Jamii Bibi Felister Mdemu, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Familia ya Watu 11 wenye ulemavu wa Macho katika Kituo cha Buigiri Jijini Dodoma leo Disemba 31,2020 kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya, ambapo Makamu wa Rais amewatakia Watanzania wote Kheir na Baraka ya mwaka mpya 2021 na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutuvusha salama mwaka 2020 na kutufikisha salama mwaka mpya wa 2021 na kuutakia mwaka 2021 uwe wa kheir, Baraka na mafanikio kwenye malengo yetu. pamoja na kuwaomba Watanzania kumuomba Mwenyezi Mungu ili atuepushe na kila janga katika Nchi yetu, nawaomba tuendelee kuchapa kazi. Kheir ya mwaka mpya wa 2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 

No comments:

Post a Comment