Pages

Thursday, December 31, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE KATIKA MAKAO MAKUU YA SEKRATARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Desemba, 2020 amewasilisha fomu zake za maadili katika ofisi ya makao makuu ya Sekratarieti ya Maadili ya viongozi Jijini Dodoma.

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike amekabidhi fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili, Jaji wa

Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi.

Leo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maadili kwa viongozi wote kwa mujibu wa Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ya Maadili ya Viongozi wa Umma

 

No comments:

Post a Comment