Na Mwandishi Wetu,
Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani, amewaagiza watendaji wa Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijjini (REA),
kuhakikisha wanawaunganishia umeme wateja wote waliolipia ankara za
umeme jijini Mwanza na maeneo ya vijijini ndani ya miezi mitatu kuanzia
tarehe 30 Desemba, 2020.
Waziri
Kalemani ameyasema hayo, tarehe 29 Desemba, 2020, alipokuwa akizungumza
na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) katika kikao kazi cha pamoja kilichofanyika
kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza.
Pamoja
na agizo hilo la kuwaunganishia umeme wateja hao ndani ya miezi mitatu,
Waziri Kalemani, amewaelekeza watendaji hao kuhakikisha wateja wote
walioko katika maeneo ya vijijini na kando kando ya miji,
wanaunganishiwa umeme kwa gharama ya Shilingi 27,000 bila kujali umbali
wa mita 30 kwani ni wajibu wa TANESCO kuwafikishia wananchi nguzo za
umeme ili kuwafikia wateja hao.
“Mnataka
kila mwananchi awe mita 30 ndipo muwafikishie umeme? Ni kazi yenu
kupeleka nguzo hadi muwafikie wananchi hao. Nisisikie mtu anaongelea
suala la mita 30.” amesema Kalemani
Vilevile,
Waziri Kalemani, ameitaka TANESCO kuanzisha madawati ya huduma kwa
wateja ili kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma bora na kwa wakati ili
kuwaondolea adha ya kufuatilia maombi ya kuunganishiwa umeme kwenye
Ofisi za TANESCO wilayani.
Amewataka
watendaji wa TANESCO kuwafuata wateja mahali walipo na kuepuka kutumia
lugha ya kukatisha tamaa kwa wateja ili kujenga mahusiano mazuri na
wateja jambo litakalopelekea kupanua wigo wa wateja na kuongeza mapato
kwa Shirika.
”
Masurveyor ndio wanaolalamikiwa sana kwa kutoa lugha zinazokatisha tama,
ninawasihi mbadilike kuanzia sasa, atakayebainika anatumia lugha mbaya
kwa mteja, huyo tutaachana naye na atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Wateja wote wahudumiwe bila kubaguliwa, tunataka wateja wote wapate
umeme bila kubaguliwa.”Amesema Dkt. Kalemani
Aidha,
Dkt. Kalemani, amewapongeza watumishi wa TANESCO kwa utendaji mzuri na
kueleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 80 utendaji wa TANESCO ni wa
Kuridhisha.
Waziri
Kalemani pia ameelekeza watumishi walioajiriwa kwa muda, wanaohusika na
kazi za kupimia wananchi maeneo ya kuunganisha umeme, wanunuliwe
pikipiki zitakazowawezesha kuwafikia wateja kwa urahisi.
Vilevile,
Waziri Kalemani amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kasi, ubunifu
na kwa usahihi na amewataka watumishi wa TANESCO na REA kujiepusha na
vitendo vya rushwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika kikao kazi hicho, Naibu Waziri wa
Nishati, Mhe. Stephen Byabato, amewataka watumishi wote kuzingatia
maelekezo yaliyotolewa na Waziri Kalemani, na kueleza kuwa atahakikisha
anasimamia na kufuatilia utekelezaji wake kwa ukamilifu.
Kikao
kazi baina ya Waziri Kalemani na watumishi wa TANESCO na REA, ni kikao
kazi cha pili baada ya kufanya kikao na wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa
Geita wiki iliyopita. Lengo la vikao hivyo ni kuweka misingi ya pamoja
ya utendaji kazi unaolenga kuleta matokeo chanya na ya haraka katika
Sekta ya Nishati.
No comments:
Post a Comment