Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kupanga maandamano.
Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless Lema, na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo.
Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa wamepanga kuanza maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo
Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo polisi wamesema ni ya vurugu. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa chama cha ACT Wazalendo.
No comments:
Post a Comment