Na John Walter-Babati, Manyara
Siku chache baada ya Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli kutoa agizo kwa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Manyara kuwaunganishia Umeme Wananchi ambao bado hawakufikiwa na Huduma hiyo ndani ya Siku 30, Afisa Uhusiano na wateja TANESCO Mkoa wa Manyara Marcia Simfukwe, amesema utekelezaji umeanza.
Simfukwe amesema ndani ya siku zilizotolewa na Rais Magufuli,
wana uhakika wa kukamilisha agizo hilo na kwamba zoezi limeshaanza na
hatua ya awali ni kusambaza nguzo kwa wananchi.
Afisa huyo amewaomba wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki
walichopewa na watoe ushirikiano wa kutosha kwao ili kukamilisha zoezi
hilo kwa muda mfupi.
Amesema katika mkoa wa Manyara kuna wilaya tatu zinazohudumiwa
na TANESCO mkoani hapo ambazo ni wilaya za Hanang, Mbulu na Babati
ambazo zote tayari zina watumishi wa kutosha kutoka shirika hilo huku
wengine wakitoka mikoa ya jirani ili kukamilsha zoezi hilo kwa wakati.
Pia amesema umeme huo wa REA utaifikia kila nyumba kwa gharama ya shilingi elfu 27, 000 pekee bila kujali wingi wa nguzo zinazohitajika.
Oktoba 25,2020 Dkt Magufuli akiwa katika Kampeni za Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Kwaraa Mjini Babati mkoa wa Manyara, alimuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Manyara Mhandisi Rehema Hussein Mashinji kusambaza Umeme kwa wananchi 4000 ambao tayari wamekidhi vigezo vya kupatiwa umeme huo ndani ya siku 30.
No comments:
Post a Comment