Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike 'Kipepeo Pad' Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi
wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha na shule ya Msingi
Ushirika.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi
wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo katika kata ya
Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 2,2020 katika shule
ya msingi Ushirika. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akionesha taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), kwa
ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo
katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akionesha taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilizotolewa na Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), kwa
ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo
katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Muonekano
wa sehemu ya taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa ajili ya wanafunzi
wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya sekondari
Chamaguha zilizotolewa Kampuni ya APS.
Muonekano
wa sehemu ya maboksi yenye taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa ajili ya
wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya
sekondari Chamaguha zilizotolewa Kampuni ya APS.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo
za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi
Ushirika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Chamaguha, Irene Mshandete.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
akielezea lengo la kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika
shule ya msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha kuwa ni
kusaidia kupunguza utoro shuleni kwani baadhi ya wanafunzi wa kike
wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo za kike wanapokuwa
katika hedhi.

akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambayo pia alisoma
wasome kwa bidii.
Waliowahi
kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika walioambatana na Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi
Ushirika wakiwa wamekaa. Wa kwanza kushoto ni Zubery Bundala akifuatiwa
na Agnes Mambosasa, Eva Laurent na Sara Elias.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
na Sara Elias wakipiga picha na wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
na Sara Elias wakiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
na waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika wakipiga picha
ya kumbukumbu na wanafunzi na mmoja wa walimu wa muda mrefu wa shule
hiyo baada ya kutoa taulo za kike.
Kushoto
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co.
Ltd), Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike 'Kipepeo Pad' Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi
wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha iliyopo katika kata ya
Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 2,2020 katika shule
ya Sekondari Chamaguha.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
akionesha na kuwaelezea wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari
Chamaguha namna taulo za kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
akiwaonesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za
kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu
akiwaonesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za
kike 'Kipepeo Pad' zilivyo bora.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.

Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike.
Afisa Elimu Sayansi Kimu na Afya Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike
Mkuu wa shule ya sekondari Chamaguha, Komanya Mathias Busasi akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike
Wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakionesha Taulo za kike 'Kipepeo Pad'
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya
APS, Viongozi wa kata ya Chamaguha, Manispaa ya Shinyanga, walimu na
wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakipiga picha ya kumbukumbu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu akiagana na Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) baada ya zoezi la
kugawa Taulo za kike 'Kipepeo Pad' kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma
katika shule ya Sekondari Chamaguha na shule ya Msingi Ushirika.Kampuni
ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company) inayojihusisha
na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike maarufu kwa jina
Kipepeo Pad imetoa msaada wa taulo za kike 400 kwa wanafunzi 30
wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na
shule ya Sekondari Chamaguha zilizopo katika kata ya Chamaguha Manispaa
ya
Shinyanga.
Hafla fupi
ya makabidhiano ya Taulo za kike ‘Pedi’ imefanyika leo katika shule ya Ushirika
na Chamaguha na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu aliyeambatana na baadhi ya waliokuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe.
Jasinta Mboneko.
Akizungumza
wakati wa kupokea Taulo hizo za kike kutoka Kampuni ya APS, Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko aliishukuru Kampuni ya APS kwa msaada huo
akibainisha kuwa zitasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa katika hedhi.
“Asanteni
sana APS Company kwa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi 10
wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na wanafunzi 20 wanaosoma katika
shule ya sekondari Chamaguha watakazozitumia kwa muda wa mwaka mmoja. Hakika
mmeunga mkono kwa vitendo kampeni yetu ya
‘Msitiri msichana,punguza utoro shuleni’ tuliyoianzisha hivi karibuni”,amesema Mboneko.
“Tunakushukuru
ndugu yetu Janeth Dutu kupitia Kampuni yako ya APS pamoja na waliowahi kuwa
wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambao umeambatana nao leo kuleta taulo za
kike. Hii ni sadaka kubwa mmetoa”,ameongeza Mboneko.
Mkuu huyo wa
wilaya ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia upatikanaji
wa taulo za kike shuleni kwani bado wanafunzi wa kike wanapata changamoto akieleza
kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.
Katika hatua
nyingine Mboneko amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuepuka vikundi viovu
na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kukatisha ndoto zao.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS), Janeth
Dutu amesema lengo la kutoa taulo za kike ni kupunguza utoro shuleni kwani
baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo
za kike wanapokuwa katika hedhi.
Amesema
kutokana na uwepo wa taulo za kike wanafunzi watahudhuria masomo yao hata kama
wapo katika hedhi hivyo ufaulu wao utaongezeka.
“Ninaamini
kabisa taulo zetu za kike zinazojulikana kwa jina la Kipepeo Pad ambazo zina
ubora wa hali ya juu zitawasaidia wanafunzi 10 katika shule ya msingi Ushirika
ambayo nilisoma lakini pia wanafunzi 20 katika shule ya sekondari Chamaguha
ambapo nitaendelea kuwahudumia wanafunzi hawa kwa muda wa mwaka mmoja”,amesema
Janeth.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi walionufaika na msaada
huo, Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha ameishukuru Kampuni
ya APS kwa kuwapatia taulo za kike akieleza kuwa awali walikuwa wanalazimik kutumia
vitambaa na wakati mwingine baadhi yao kuwa watoro shuleni pindi wanapokuwa
katika hedhi
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment