Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli za treni ya abiria itakayofanya safari zake kutoka Moshi mjini hadi Arusha na kurudi Moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo tarehe 29 Septemba, 2020, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema nauli hizo zimetangazwa kufuatia
Shirika la Reli Nchini (TRC) kuwasilisha maombi ya nauli hizo, ambapo LATRA ilifanya mikutano ya kupokea maoni ya wadau, kisha kufanya uchambuzi wa maoni hayo pamoja na kuchambua mchanganuo uliowasilishwa na TRC.Kwa mujibu wa kifungu cha 21 (2) (b) cha Sheria ya LATRA namba 3 ya 2019, baada ya mchakato wa uchambuzi kukamilika, Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA imeidhinisha nauli hizo na kuainisha nauli zitakazotumika kwa usafiri wa treni ndani ya mikoa hiyo na nje ya mikoa kama inavyoonekana katika jedwali.
Nauli zilizoidhinishwa na LATRA zikionesha mchanganuo wa vituo vya ndani nan je ya mikoa husika
KUTOKA MOSHI KWENDA | Umbali (KM) | NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS): | ||
Daraja la tatu | Pili kukaa | |||
1 | RUNDUGAI | 22 | 1,000 | 1,500 |
2 | KIKULETWA | 31 | 1,000 | 1,500 |
3 | KIA | 37 | 1,000 | 1,500 |
4 | USA RIVER | 62 | 1,500 | 2,000 |
5 | TENGERU | 65 | 1,500 | 2,000 |
6 | CHEKERENI | 75 | 1,500 | 2,000 |
7 | NJIRO | 82 | 1,500 | 2,000 |
8 | ARUSHA | 86 | 1,500 | 2,000 |
KUTOKA ARUSHA KWENDA | Umbali (KM) | NAULI KWA MADARAJA HUSIKA (SHS): | ||
Daraja la tatu | Pili kukaa | |||
1 | NJIRO | 4 | 1,000 | 1,500 |
2 | CHEKERENI | 11 | 1,000 | 1,500 |
3 | TENGERU | 21 | 1,000 | 1,500 |
4 | USA RIVER | 24 | 1,000 | 1,500 |
5 | KIA | 49 | 1,500 | 2,000 |
6 | KIKULETWA | 55 | 1,500 | 2,000 |
7 | RUNDUGAI | 64 | 1,500 | 2,000 |
8 | MOSHI | 86 | 1,500 | 2,000 |
Nauli za wanafunzi kutoka mwanzo hadi mwisho wa safari ni Sh. 300.00 kwa daraja la tatu, na Sh 400.00 kwa daraja la pili kukaa.
Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe akimkabidhi Henry Machoke, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TRC andiko la nauli zilizoidhinishwa
Wakati huo huo, LATRA imeiagiza TRC kutekeleza masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya usalama kwa wadau husika, kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki, kutoa ratiba za safari kwa umma, kutekeleza hatua za usalama kudhibiti msongamano wa abiria, kuboresha miundombinu na huduma za kijamii, kuweka kitengo cha huduma kwa wateja na kutangaza nauli zilizoidhinishwa katika vyombo mbalimbali vya habari ili ziwafikie wadau wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment