*****************************************
Na Mwandishi Wetu, Mtwara.
Katika
kuhakikisha azma ya Serikali ya kuendeleza na kukuza uchumi wa Viwanda,
Kituo cha
Uwekezaji Tanzania-TIC kimesema ipo haja kwa Wawekezaji
kukitumia kituo hicho katika kufanikisha shughuli zao ambazo ndio chachu
ya ukuaji wa uchumi huo.
Kituo hicho
ambacho kinaratibu, kuhamasisha na kusimamia Uwekezaji nchini sasa
kinafanya jitihada za kuwatembelea Wawekezaji kwenye maeneo ya uwekezaji
wao ili kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi wa
Kituo hicho Dkt Maduhu Kazi aliwatembelea Wawekezaji Mkoani Mtwara
ambapo akiwa katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote,alisema lengo ni
kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na Wawekezaji pamoja
na Wadau wa Sekta mbalimbali za Serikali na Binafsi zinazohusika na
uwekezaji katika kufanikisha shughuli hizo nchini.
“Nawapongeza
sana Wawekezaji wa Kiwanda hiki cha Dangote, mnafanya kazi nzuri katika
uwekezaji wenu, sisi TIC tupo kwa ajili yenu, kitumieni kituo hiki kwa
maendeleo ya Uwekezaji katika nchi yetu na sisi tupo tayari kuwahudumia
wawekezaji wote ili kukidhi matarajio ya nchi katika ukuaji wa uchumi”
alisema Dkt Kazi.
Meneja Mkuu
wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Bw. Aboyomi Awofodu amesema kwa sasa
kiwanda hicho kinafunga mitambo ya kisasa itakayowezesha kutumia umeme
wa gesi, makaa ya mawe na maji ili kuwa na umeme wa uhakika wakati wote.
Kiwanda cha
Saruji cha Dangote chenye eneo la ekari 1,700 kilichopo katika eneo la
Msijute katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ni moja ya Uwekezaji
Mkubwa Nchini Tanzania, Kiwanda hiki ni kikubwa katika eneo la Kusini
mwa Jangwa la Sahara na kina uwezo wa kuzalisha tani za saruji milioni
tatu kwa mwaka.
Kiwanda hiki
kilianza kazi Desemba 2015 na hadi sasa kiwanda hicho kinazalisha saruji
ya kiwango cha daraja la 32.5 na 42.5 ambayo inatumika nchini na
nyingine kusafirishwa nje ya nchi, hivi karibuni Waziri wa Nishati Dkt
Medard Kalemani alizindua mradi wa kwanza wa kuunganisha miundombinu ua
gesi asilia katika kiwanda hicho kwa ajili ya kuzalisha umeme wa
megawati 45, Mmiliki wa kiwanda hicho ni Raia wa Nigeria Alhaj Aliko
Dangote.
No comments:
Post a Comment