Meneja
wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi akizungumza kwenye kongamano
la wadau wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATO) lililowaleta pamoja zaidi ya
wadau 250 katika Hoteli ya Verde.Meneja
wa matawi ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi (kushoto) akimkabidhi hotuba
yake Waziri wa Fedha Zanzibar- Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa aliyekua
mgeni rasmi katika kongamano la Wadau wa Utalii Zanzibar. Kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Kadi wa NMB – Philbert Casmir.
************************************
Benki ya NMB imesema kuwa
inathamini sana sekta ya utalii nchini na imeweka mikakati endelevu
zaidi katika
kuhakikisha shughuli za utalii zinakuwa zaidi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa
matawi ya Benki ya NMB Zanzibar – Abdalla Duchi, wakati wa mkutano wa
wadau wa utalii Zanzibar(ZATO) uliofanyika visiwani humo kwa udhamini
mkuu wa Benki ya NMB.
Alisema Benki hiyo imejipanga
vyema kutoa suluhisho la huduma za kifedha, kwa kuwa na mifumo bora
zaidi ikiwemo ya ubadilishaji fedha na Biashara ya kadi
ambayo imewezesha wataliii kutohangaika wanapofanya manunuzi na malipo
mbali mbali kwa kushirikiana na mahoteli na baadhi ya makampuni ya
utalii, walihakikisha wana mashine za malipo (POS) na pia kuimarisha
mfumo wa malipo ya mitandano (E-Commerce).
Naye Mkuu wa Idara ya Biashara
za kadi wa Benki ya NMB – Philbert Casmir alisema wanaimarisha huduma
hizo ili kuhakikisha watalii wanapata huduma kupitia matawi ya Benki hio
hasa pale yanapotokezea majanga ikiwemo Covid – 19 ambayo ilisitisha
huduma nyingi.
Philbert Alifafanua kuwa Benki
hiyo inaelewa katika kipindi cha Covid -19 biashara ikiwemo ya utalii
na sekta ya hoteli zilipata changamoto. Hivyo, NMB ipo karibu zaidi na
wateja wao ili kuhimili changamoto hizo zilizojitokeza.
Ametoa rai kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, wajumbe wa ZATO, na Wananchi wa Zanzibar kwa
ujumla, kutumia Benki ya NMB kwani ipo kwa ajili yao, na ina mifumo
thabiti ya kutoa suluhisho la huduma za kibenki, na ndiyo maana
imetambuliwa na taasisi za kimatafa kama EURO Money kuwa ndio benki bora
zaidi hapa nchini kwa miaka minane mfulululizo.
No comments:
Post a Comment