Mkurugenzi
mtendaji wa TASAF Nchini Satanslaus Mwamanga akizingumza katika kikao
cha kazi cha kujengea uwezo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji
wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN)
Katibu
Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizingumza katika kikao cha
kazi cha kujengea uwezo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa
kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF (PSSN)
Mwenyekiti
wa muda katika kikao hicho kwa kuchaguliwa na wajumbe ndugu Bahati
Nyakiraria akitoa neno la shukrani mara baada ya mgeni rasmi kufungua
kikao hicho leo katika ukumbi wa Arusha DC leo augusti 2020-01 septemba
2020
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kujenga uelewa kwa
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya
tatu ya TASAF (PSSN II)
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao hicho cha kujenga uelewa kwa
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya
tatu ya TASAF (PSSN II)
====== ====== =====
Na Vero Ignatus,Arusha
Kaya
1320 zimetajwa kuomba kujiondoa kwenye mpango wa kuhudumia Kaya
masikini TASAF katika mkoa wa Arusha wakati serikali ikipanga kutekeleza
mpango huo kipindi cha pili awamu ya Tatu kutokana na kujikwamua
kiuchumi baada ya kuwezeshwa na TASAF.
Idadi
ya Kaya hizo kujitoa katika mpango huo umeelezwa na Mkurugenzi wa TASAF
Ladislaus Mwamanga wakati wa Kika kazi Cha kujenga uelewa kwa Waandishi
wa habari kuhusu utekelezaji wa mpango huo kipindi Cha ili awamu ya
Tatu unaotarajiwa kuanza Mara badaa ya Uchaguzi Mkuu kupita
Akizungumza
kwenye kikao kazi hicho Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga
alisema kuwa dhamira kubwa yaa Tasaf ni pamoja na kuupunguza umasikini
kwa kuzingatia uwazi uwajibikaji,na ushirikishwaji wa katika kuleta
Maendeleo.
Mwamanga
amesema kuwa mpango huo umewezesha utoaji ajira za muda katika
halmashauri 42 Tanzania bara na Tanzania zanzibar ambapo jumla ya miradi
7,775 imetekelezwa katika vijiji,mitaa na shehia 1,928 na kufikia jumla
ya walengwa 253,117 kwa kupata ajira za muda
Utekelezaji
wa TASAF awamu ya kwanza jumla ya miradi 1,704 ilitekelezwa na jamii
yenye thamani ya shilingi Bilioni 72 kwenye halmashauri 40 Tanzania bara
na Zanzibar ambapo miradi 1,338 ya huduma za jamii ,miradi 61 ya
makundi maalum na miradi 305 kutoa huduma za muda
Kwa
awamu ya pili jumla ya miradi 12,347 yenye thamani ya shilingi bilioni
430 ilitekelezwa na jamii katika halmashauri 126,miradi 4,297 ya huduma
ya jamii kutoka sekta zote,miradi 6,260 makundi maalum,miradi 1,790 ya
kutoa ajira za muda yenye walengwa 152,458,vikundi 2,778 vya kuweka
akiba na kuwekeza nyenye wanachama 27,800, ambapo utekelezaji wa miradi
hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa haswa katika sekta za elimu,Afya,Maji
na barabara za vijijini
Katika
awamu ya tatu jumla ya kaya milioni 1.3 zilitambuliwa katika
halmashauri zote za Tanzania bara na Zanzibar (Unguja na Pemba)Jumla ya
kaya maskini milioni 1.1 zenye watu takribani milioni 5 ziliandikishwa
na asilimia 52 ya walengwa ni wanawake ,mpango huo ulitekelezwa katika
jumla ya vijiji,mitaa na shehia 9,986 ambapo jumla ya shilingi bilioni
968.7 zimetumika kwa walengwa wa mpango mpaka februari 2020
Akieleza
chagamoto ambazo wanakutana nazo uwepo wa vijiji ,mitaa na shehia
nyingi zenye kaya maskini ambazo hazijafikiwa kwasababu ya upungufu wa
rasilimali fedha 30%ya vijiji ,mitaa na shehia,ukosefu wa fedha kwaajili
ya kutekeleza miradi ya jamii kuboresha miundombinu,kuwepo kwa kaya
ambazo siyo maskini kwenye mpango
Akifungua
kikao kazi hicho mgeni wa heshima ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa
Arusha Richard Kwitega amepongeza hatua ya mfuko huo wa kuhudumia kaya
masikini nchini TASAF kuanza mpango kwa kushirikisha waandishi wa habari
kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira
husika.
hata
hivyo amewashauri waandishi wa habari kuzingatia uweledi wakati wa
kuripoti hatua mbalimbali za mpango huo ili kutojenga taharuki ya
kiuelewa kwa jamii na walengwa wenyewe lakini pia na kuepuka
upotoshwaji.
Hata
hivyo serikali ilianzisha Mfumo wa Maendeleo kwa Jamii (TASAF) mwaka
2000 kwa madhumuni ya kusaidiana na vyombo vingine vya serikali
kupunguza umaskini,ambapo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika
ngazi za jamii kwa lengo la kutoa huduma za kijamii katika sekta zote
kwa kuzingatia mahitaji halisi au kero za wananchi na imetekelezwa kwa
awamu tatu.
No comments:
Post a Comment