Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa LSF, Beng’i Issa,akizungumza wakati wa Mkutano wa
shirika hilo unafanyika kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo
ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara
na Zanzibar jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu
wa Shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF), Lulu
Ng’wanakilala,akizungumza wakati wa Mkutano wa shirika hilo unafanyika
kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo
yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini
Dodoma.
Sehemu ya washiriki
wa Mkutano wa shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini
(LSF),wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa leo.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika la Kilimajaro Women Information Exchange Community
Organization Bi.Elizabeth Minde akitoa mada kwenye Mkuu wa shirika la
kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF) unafanyika kwa siku tatu
ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya
msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
Mjumbe wa
Bodi,Jenitha Kangura ,akizungumza kwenye Mkuu wa shirika la kutoa
msaada wa Kisheria nchini (LSF) unafanyika kwa siku tatu ulikutanisha
mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa
kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Migogoro ya ardhi na
dhuluma za mirathi kwa wajane ni migogoro inayohitaji msaada mkubwa wa
kisheria nchini kwani imekuwa ikiripotiwa kwa wingi kwa watoa huduma za
msaada wa kisheria.
Inasemekana migogoro
hiyo imekuwa ikitajwa kama tatizo kubwa linalohitaji angalizi wa karibu
wa msaada wa kisheria ili kuweza kupungza migogoro hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa
leo Jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la kutoa msaada wa
Kisheria nchini (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakati akizungumza na
waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wa shirika hilo.
Mkutano huo
umeyakutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma
ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.
Ng’wanakilala
ameeleza eneo ambalo linahitaji “Sisi jukumu letu ni kutoa msaada wa
kisheria bure nchi nzima na kwa miaka nane ambayo shirika limekuwa
likifanya kazi zake tumeona eneo ambalo linahitaji msaada mkubwa wa
kisheria ni kwenye ardhi kuna migogoro mingi huko.”
Ng’wabakilala
amesema wamekuwa wakipata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake ambao
wanadhulumiwa mali na mirathi yao baada ya wenza wao kufariki dunia.
Hata hivyo amesema
kuwa shirika hilo pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa watu wote
lakini limejikita zaidi katika kutoa msaada kwa wanawake ambao kwa kiasi
kikubwa ndiyo waathirika wa kudai haki baada ya kudhulumiwa.
Kwa upande wake
Meneja ufuatiliaji matokeo wa shirika hilo Said Chitung amesema
kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa watu wanaohitaji msaada wa kisheria
waliamua kutoa mafunzo kwa watoa msaada wa kisheria 4,031.
Kwa kuongezea
ameeleza kuwa idadi hiyo ni ndogo kulinganisha na uhitaji uliopo kwani
lengo lao ni kuwa na watoa msaada wa kisheria 6,000 nchi nzima ili
kukidhi mahitaji yaliyopo.
Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa LSF, Beng’i Issa ameyataka mashirika hayo
kuwafikia watu ambao wanataka kujishughulisha kwenye miradi ya kimkakati
nchini na hawajui pa kuanzia.
Amesemakwa hivi sasa
serikali inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli
ya kisasa, bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere lakini watu wengi
hawajui jinsi ya kushiriki kwenye miradi hiyo kwa kuwa hawajui sheria
inayowalinda
No comments:
Post a Comment