Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano
Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa
huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni
ulioandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na UCSAF uliofanyika leo Agosti
31,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza . Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akizungumza katika Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya
Ziwa.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akielezea kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na UCSAF.
Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana Jengela akitoa mada kuhusu uanzishwaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na malengo ya mfuko huo.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji UCSAF, Albert Richard akielezea kuhusu miradi
mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Wadau wa
mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio,
Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma
ya maudhui mtandaoni wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TCRA na
UCSAF.
Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu
wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi
ya UCSAF akiwahamasisha watoa huduma za mawasiliano kuungana kuomba
ruzuku kujenga minara ili kuongeza usikivu wa vyombo vyao vya habari
kwenye maeneo yasiyosikika. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala
UCSAF, Pius Joseph. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji
UCSAF, Albert Richard akifuatiwa na Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana
Jengela.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi wa Malunde Media ‘Malunde 1 blog’, Kadama Malunde akiwa ukumbini.
Mkurugenzi
wa Malunde Media ‘Malunde 1 blog’ , Kadama Malunde (kulia) na Estomine
Henry kutoka Shinyanga Press Club blog wakiwa ukumbini.
Wadau wa
mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio,
Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma
ya maudhui mtandaoni wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TCRA na
UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini

Maafisa wa TCRA Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano
kwa wote (UCSAF) umekutana na wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa
wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za
usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa lengo
la kuwajengea uelewa watoa huduma na wadau hao kushiriki shughuli za
mfuko wa UCSAF na kutimiza wajibu wao kisheria.
Akizungumza
katika Mkutano huo leo Agosti,31 2020 uliofanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala
UCSAF, Pius Joseph alisema mkutano ulilenga kuwajengea uelewa wadau wa
mawasiliano namna mfuko wa UCSAF unavyofanya kazi na wajibu wao
kisheria.
Joseph aliyataja miongoni mwa
mafanikio yaliyofikiwa na mfuko wa UCSAF ni pamoja na kufikisha huduma
ya mawasiliano ya simu katika kata 631 kati ya kata 994 zilizosainiwa
mkataba,ufikishwaji wa matangazo ya runinga ya kidigitali katika mikoa
ya Katavi, Geita,Simiyu,Njombe na Songwe pamoja na ujenzi wa vituo 10
vya TEHAMA Zanzibar na 11 Tanzania bara ambapo kituo kimoja kimejengwa
katika kila wilaya.
Hata hivyo alisema suala la
ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi unaathiri kasi ya mfuko kufikisha
mawasiliano,ukosefu wa fedha za kutosha kufikisha mawasiliano kwa
kipindi kifupi zaidi kulingana na mahitaji na uelewa wa watoa huduma na
wadau mbalimbali kushiriki shughuli za mfuko na kutimiza wajibu wao
kisheria.
Joseph aliwashauri wamiliki wa
vituo vya utangazaji kushirikiana kujenga minara ya pamoja ili kupunguza
gharama za kuendesha vituo vya matangazo na kwamba UCSAF inachofanya ni
kuwawezesha watoa huduma kwa kuwapa ruzuku ili kujenga minara.
Kwa upande wake, Mkuu wa TCRA
Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya UCSAF
alisema upenyo wa kuenea kwa vyombo vya habari kanda ya Ziwa bado
hauridhishi ambapo usikivu wa redio Kanda ya Ziwa upo chini ya asilimia
50 hivyo kuwaomba Watoa huduma za mawasiliano kuomba Ruzuku UCSAF kwa
ajili ya kujenga minara ya pamoja ili walau usikivu ufikia asilimia 60.
“Mkijenga minara maeneo
mengine,kama kuna mnara umejengwa na wadau wa sekta ya
utangazaji,gharama zitapungua. Tuache ubinafsi tutumie minara
iliyojengwa kwa ruzuku ya serikali. Lengo tunataka kuongeza usikivu wa
radio Kanda ya Ziwa”,alisema Mhandisi Mihayo.
“Kuna watu wanawafanya nyinyi
kama vitega uchumi, akili kubwa mnaelekeza kulipia kodi ya minara ili
msizimiwe matangazo,hao wanaowapangisha silaha yao kubwa ni kuzima
matangazo. Nawasihi wamiliki wa vituo vya utangazaji kuungana.
Tumieni nafasi hii mji –
organize, leteni maombi UCSAF kujenga mnara wa pamoja ili kupunguza
gharama za uendeshaji wa vituo vyenu tuache wivu na ubinafsi. Jengeni na
kumiliki vya kwenu kupitia ruzuku ya serikali, tunataka mjenge wote,
utakachotakiwa kufanya ni utachangia umeme na kulipa mlinzi tu”,aliongeza Mihayo.
Hata hivyo Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla alisema
lengo la UCSAF kuhamasisha watoa huduma za mawasiliano kujenga minara
ya pamoja ni kutaka kupeleka matangazo sehemu ambazo hakuna mawasiliano.
“Sasa hatuangalii pale ulipo,tunaangalia kule ambako
hufiki,kule unapotakiwa kupeleka mawasiliano ili kuboresha zaidi huduma
za mawasiliano”,alisema Nyalla.
Miongoni mwa maazimio
yaliyofikiwa na washiriki wa mkutano huo ni pamoja na kulipa tozo kwa
mujibu wa sheria,maombi ya mnara kwenye maeneo husika ufanywe na watoa
huduma za radio na TV kupitia wawakilishi waliopo katika mkoa husika na
mnara unapoanzishwa utumike kwa watoa huduma watakaohitaji kwa kulipia
ghrama za umeme na ulinzi na UCSAF ujikite kutoa elimu ya mfuko na
wajibu wa watoa huduma za mawasiliano.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment