KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony
Sanga akizungumza na watendaji wakuu wa idara za Maji wakati kikao kazi
cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji kilichofanyika leo
jijini Dodoma .
Sehemu ya washiriki
wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony
Sanga akizungumza na watendaji wakuu wa idara za Maji wakati kikao kazi
cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji kilichofanyika leo
jijini Dodoma .
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara
ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa wito kwa watendaji wakuu wa idara
za Maji kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia lengo la kuwahudumia
wananchi.
Aidha wito huo
umetolewa leo kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya
Maji Mhandisi Sanga amesema kuja baadi ya watendaji wanafanya kazi bila
ushirikiano hali ambayo inaounguza tija katika kutoa huduma hiyo kwa
wananchi.
“Maeneo mengi bado
kuna umimi,naomba umimi huu tuumalize,tushirikiane katika utendaji wetu
kwa ajili ya kufanya kazi yetu iwe bora zaidi katika kuwatumikia
wananchi.” Amesema Mhandisi Santa
Mhandisi Santa amesisitiza kuwa watendaji hao kila mmoja kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana katika eneo lake .
Pia amewataka
kusimamia miradi ya Maji inayongwa na kuhakikisha inajengwa kwa ubora na
kwa thamani ya fedha inayotumuka katika mradi husika.
“Miradi msingi hivi
sasa tunaitekeleza kwa fedha za” force account” sasa kama mradi unapaswa
kukaa miaka 50 na iwe hivyo siyo mradi unajengwa kwa kutumiabfefha
nyingi halafu baada ya muda kidogo unakuwa na nyufa,hii siyo
sawa”ameongeza Mhandisi Santa
Naye Katibu Mkuu
Utumishi Dkt Francis Michael amesema watumishi wa Umma nchini hawana
budi kuzingatia maadili ya utumishi Wa Umma na kuepuka mihemuko ya
Kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28
mwaka huu.
” Tunaelekea kwenye
kipindi Cha Uchaguzi lazima tujue majukumu yetu nini sisi Kama watumishi
wa umma hilo lazima kila mtumishi kulitambua bila kusahau uwadilifu,”
amesisitiza Dkt Francis.
Aidha meongeza kuwa
katika suala zima la siasa watumishi wa Umma wanahaki ya kidemokrasia
kuchagua na kuchaguliwa au kuwa mwanacha wa Chama fulani Cha siasa
nchini.
Kwa upande wake Naibu
Mwanasheria Mkuu Serikalini DAG Dkt.Evaristo Longopa…….kila mtu
anahaki kikatiba kuchagua na kuchaguliwa na kutoa maoni yao.
Hata hivyo amesema
katika ibara ya 20 kwenye katiba yetu inasema raia yoyote anahaki ya
kushiriki na wenzake kwenye vikundi vya ushirika au vyama vya siasa.
“ ibara ya113 (a)
inakataza majaji na mahakimu kujiunga na Chama chochote Cha siasa kwa
sababu wenywe ndio watoa haki hivyo hawatakiwi kuwa wanachama wa Chama
Cha siasa”ameeleza .
No comments:
Post a Comment