Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Utalii
wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Kukukuza Utalii wa ndani leo jijini Dar
es salaam.
***********************************
Na. Aron Msigwa – WMU.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa watanzania
wajitokeze
kuwekeza katika biashara ya Utalii kwa kuwa masharti ya
kuwekeza katika biashara hiyo yamerahisishwa tangu Serikali ya Awamu ya
tano ilipoingia madarakani.
Dkt. Kigwangalla
ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Mkakati wa
Kukuza Utalii wa ndani unaolenga kutoa ajira na kuwahamasisha
watanzania washiriki na kuwekeza katika sekta ya utalii na
kuvitembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Amesema tangu
kuingia Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli
yamefanyika mabadiliko mbalimbali yaliyolenga kuleta tija na
kuifungamanisha sekta ya utalii na maendeleo ya watu kwa kuhakikisha
wananchi wananufaika na sekta hiyo.
Dkt. Kigwangalla
amesema Serikali ilifanya jitihada za makusudi za kulegeza masharti na
kushusha viwango vikubwa vya tozo vilivyokuwepo ambavyo vilikua
vinawazuia wafanya biashara wadogo hasa wazawa washindwe kuingia katika
sekta hiyo.
Amesema tangu kuondolewa kwa
masharti hayo watanzania wazawa wanaofanya biashara ya huduma za utalii
wameongezeka kutoka 1100 hadi kufikia 2000 wengi wao wakiwa watanzania.
No comments:
Post a Comment