Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony
Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu leo wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hoteli ya Serena
iliyopo Jijini Dar es Salaam baada ya janga la Corona kufuatia kufungwa
kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi
vya ugonjwa huo, Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na watoto, Godwin Mollel na kulia ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Wadau
wengine wa Utalii.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto Mhe.Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe.Constantine Kanyasu pamoja na Naibu Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt.Godwin Mollel pamoja na
wadau wengine wa Utalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
hafla ya kufungua Hoteli ya Serena iliyokuwa imefungwa kwa takribani
miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya
ugonjwa wa Corona
.Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza wakati wa hafla ya kufungua
rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili
kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakati wa hafla ya kufungua
rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili
kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakichukua matukio wakati wa ufunguzi rasmi Hoteli ya Serena ya jijini
Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa
virusi vya Corona.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Dkt.
Goldwin Mollel akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya
Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza
kukabiliana na mlipuko wa virusi vya CoronaNaibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony
Mavunde akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena
ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na
mlipuko wa virusi vya Corona.
*************************************
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amepongeza uamuzi wa Hoteli ya Serena wa
kufungua hoteli hiyo tangu ilipofungwa kwa ajili ya kuweza kukabiliana
na
mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona.
Amezitoa pongezi
hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati akishiriki hafla ya kufungua
hoteli ya Serena ambayo imekuwa ni muhimu katika kuwahudumia Watalii
wengi wanaotoka na kuingia kutoka Nchi za nje kabla na baada ya
kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
Amesema uamuzi huo wakufungua hoteli hiyo
unatoa ujumbe mzito Duniani kuwa Tanzania ipo salama na ipo tayari
kwa ajili ya kuwapokea Watalii.
Amesema kurudi kwa biashara hiyo kunarudisha
uhakika wa maisha ya watu takribani 450,000 ambao wameajiriwa moja kwa
moja katika sekta ya Utalii.
Amesema Ugonjwa wa Corona uliiathiri jamii
katika nyanja za kiuchumi na kijamii baada ya watu wengi kupoteza ajira
zao na wengine kuachishwa kazi kutokana na janga hilo
Amesema uamuzi huo wa Hoteli ya Serena kuifungua
hoteli hiyo kunaleta mwanga wa matumaini kwa Watanzania wanaoitegemea
Sekta ya Utalii katika kuendesha maisha yao.
” Ninawashukuru Hoteli ya Serena kwa kupeleka
ujumbe kwa Wawekezaji wetu wote ambao wanaogopa na kufunga biashara zao
kwa ajili ya Ugonjwa huo.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea
kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya Corona na kuwa
ugonjwa huo bado upo lakini hauwezi kukimbiwa ni lazima tujifunze
kuishi nao.
” Tunamshukuru sana Rais, Mhe.John Pombe
Magufuli kwa kufanya maamuzi ya kufungua anga ambapo tunaamini biashara
ya Utalii na biashara ya anga zinategemeana kwa kiasi kikubwa.
Amesema uamuzi huo umeifanya biashara ya utalii
kuweza kurejea kwa vile tayari mashirika ya ndege ya Ethiopia, Emirates,
KLM na Quatar yameanza kuja nchini.
Naye, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto, Dkt. Goldwin Mollel amewataka Wadau wa Sekta ya
Utalii ikiwemo Wamiliki wa Hoteli kuchukua tahadhari kwa kufuata
maelekezo yaliyotolewa na Wizara yake ili kuhakikisha usalama wa Wageni
na wenyeji wanaowahudumia Watalii
Akizungumzia uamuzi huo wa kuifungua hoteli hiyo
amesema inatuma ujumbe kwa Wawekezaji wengine kuwa Tanzania ipo salama
kwa i na Watanzani wapo tayari kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta
shughuli za kibiashra.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii
Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema tangu anga lilipofunguliwa
kumeonesha dalili njema ya ujio wa idadi kubwa ya watalii
” Kuna matumaini makubwa ya kupata watalii
wengi zaidi kwa mfano siku ya jana ndege ya Shirika la KLM ilitua
Uwanjaa wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) ikiwa na kabiria
200 kati ya hao 45 ni watalii waliokuja nchini kwa ajili ya kutalii”
alisema Jaji Mstaafu Mihayo.
Amesema hiyo ni dalili njema katika sekta ya
Utalii nchini, ” Miezi mitatu iliyopita tulikuwa hatupokei watalii
kabisa kwa hofu ya janga la Corona.
No comments:
Post a Comment