*****************************
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa
inashiriki maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
yanayofanyika katika Uwanja wa
Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia
tarehe 01/07/2020 hadi tarehe 13/07/2020.
Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa ya jirani mnakaribishwa kutembelea Banda letu lililopo ukumbi wa Karume ili muweze kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya Moyo.
Madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo katika banda letu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment