Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
kufuatia
kupungua kwa maambukizi ya virusi vya COVID 19 Jeshi la Magereza nchini
limefuta masharti ya katazo la
huduma ya kuwatembelea wafungwa na mahabusu na huduma mbalimbali katika magereza ikiwamo huduma ya chakula kwa mahabusu.
huduma ya kuwatembelea wafungwa na mahabusu na huduma mbalimbali katika magereza ikiwamo huduma ya chakula kwa mahabusu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma msemaji wa Jeshi la Magereza SSP
Amina Kavirondo amesema kutokana na serikali kuruhusu shughuri
mbalimbali kuendelea Jeshi la Magereza limeondoa katazo hilo kuanzia
Augusti 1, 2020.
''Jeshi
la magereza limelegeza masharti ya katazo kuanzia 01/08/2020 huduma za
kuwatembelea wafungwa na mahabusu kwa huduma mbalimbali magerezani
zimerejeshwa'' amesema Amina.
Aidha jeshi la Magereza limewataka wageni wote pamoja na kuzingatia
sheria, kanuni na miongozo ya jeshi na Wizara ya Afya wakati wa upokeaji
wa huduma hiyo wageni watatakiwa mambo ikiwamo mfungwa au mahabusu
atatembelewa na ndugu wasiozidi wawili kwa siku za jumamosi na jumapili.
Pia limebainisha kuwa mazungumzo yatatakiwa kuto zidi dakika tano na
wale wenye vibali vya kuleta chakula italazimika kuletwa na mtu mmoja
tu, pia mgeni atatakiwa kukaa umbali wa mita moja kati ya mfungwa au
mahabusu huku wakitakiwa kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka huku
likibainisha kuwa mazungumzo ya kisheria kati ya wakili na mteja wake
yasizidi saa moja.
Aidha amebainisha kuwa kwa kipindi ambacho jeshi liliweka katazo hilo
wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo baadhi ya wafungwa
kukosa haki zao ambazo zilikuwa zinahatarisha au kusababisha kusambaa
kwa virus vya corona katika magereza lakini wamekuwa wakiwaelimisha
lengo la kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment