Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Juma Mfinanga
akipokea msaada wa moja ya magari ya kubeba wagonjwa kutoka kwa
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society Bw. James Chialo. Gari moja ni
kwa ajili ya Muhimbili na jingine ni la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma. Kulia ni Balozi wa shirika hilo, Bw. Banana Zoro.
Pichani ni moja ya gari la kubeba wagonjwa.
Mwakilishi wa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Dodoma, Bw. Maxmillian Tryphone akipokea moja magari kutoka
kwa Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society Bw. James Chialo.
Wawakilishi wa Muhimbili na Hopistali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea msaada huo.
…………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (RRH) leo wamepokea msaada wa
magari mawili ya kubeba wagonjwa kutoka asasi ya Australia Tanzania
Society (ATS) kupitia Rafiki Surgical Mission.
Akipokea msaada huo, kwa niaba ya
MNH na Dodoma, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura wa MNH, Dkt. Juma
Mfinanga amesema msaada huu umekuja wakati mzuri kwani matumizi ya
magari haya hospitalini ni makubwa.
Dkt. Mfinanga ameishukuru Rafiki
Surgical Mission imekua msaada mkubwa kwa Muhimbili kwani wamekua
wakisaidia sana hasa upande wa upasuaji (plastic surgery).
“Rafiki Surgical Mission wamekuwa
msaada mkubwa kwa Muhimbili kwani wamekuwa wakisaidia kwa muda mrefu
hasa katika eneo la upasuaji. Lakini pia wamesaidia kupeleka madaktari
bingwa na wauguzi nje ya nchi ili kuwajengea uwezo. Tunawashukuru kwa
msaada huu,” amesema Dkt. Mfinanga.
Kwa upande wa mwakilishi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Bw. Maxmillian Tryphone ameshukuru
kupatiwa msaada huo kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa katika
kuendesha shughuli za matibabu hospitalini hapo.
Naye Mkurugenzi wa ATS Bw. James
Chialo amesema leo amekabidhi magari hayo na kufikisha idadi ya magari
sita ambayo wameshatoa msaada nchini na kuna magari kama hayo 10
wataleta na kuyasambaza nchini ili kusaidia sekta ya afya.
Amesema ATS kupitia Rafiki
Surgical Missions kila mwaka wamekua wakileta watalaamu wa upasuaji ili
kushirikiana na watalaamu wa hapa nchini kufanya aina mbalimbali za
upasuaji.
Balozi wa ATS, Bw. Banana Zoro
amesema amekuwa akifanya kazi na asasi hiyo katika kusaidia sekta ya
Afya nchini na kwamba ni jambo zuri kushiriki katika shughuli ya utoaji
wa msaada huo.
No comments:
Post a Comment