Meneja wa bar ya Picnic, Bodia Kaaya akisafisha meza kwa kutumia dawa,
Meneja wa bar ya Picnic akimwagia mteja sabuni anawe mikono kabla ya kuingia Ndani ya bar hiyo kupata huduma
……………………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza,Arusha
Uongozi wa bar
maarufu ya picnic iliyopo katikati ya jiji la Arusha umeelezea mikakati
mbalimbali ambayo wanaitekeleza kipindi hiki katika kupambana na janga
la ugonjwa hatari wa corona.
Akizungumza na
waandishi wa habari meneja wa bar hiyo, Bodia Kaaya alisema kwamba
kufuatia janga la corona wao kama watoa huduma wamechukua hatua
mbalimbali kama kuhakikisha wahudumu wao wanavaa barakoa muda wote
wakati wa kutoa huduma.
Kaaya,alisema kwamba
mbali na barakoa pia wamehakikisha wameweka ndoo za maji na sabuni
katika milango ya kuingilia ndani ya eneo lao ili kunawa mikono yao
kabla hawajaingia kupata huduma.
Alisema kwamba
wametoa vitakasa mikono lakini pia wanapulizia dawa katika meza
mbalimbali zilizopo ndani ya eneo lao kama njia mojawapo ya kupambana na
corona.
Pia alisisitiza
wanafuata kanuni zote zilizotolewa na wizara ya afya nchini ambapo
wanawafundisha watumishi wao namna ya kuchukua tahadhari na ugonjwa wa
corona.
“Tunachukua tahadhari
zote tunazoelekezwa na wizara ya afya lakini pia tunawafundisha
wafanyakazi wetu namna ya kujikinga na gonjwa hili”alisema meneja huyo
Naye mtumishi wa bar
hiyo,Elisante Charles alisema kwamba wao kama watumishi wameelekezwa
hatua zote za kuchukua kujikinga na gonjwa la corona kama kuvaa barakoa
muda wote wawapo kazini.
Charles, alisema
kwamba baadhi ya watumishi wa afya wamekuwa wakipita mara kwa Mara
katika bar hiyo na kuwapa elimu mbalimbali na kufanya ukaguzi na kuiomba
serikali kufanya hivyo kwenye maeneo mengine
“Witumishi wa idara
ya Afya hapa Arusha wametupatia semina ya kutosha namna ya kujikinga na
corona wakati wa kutoa huduma pia vifaa vipo vya kutosha uongozi
umezingatia hilo na kufanya kazi kuwa rahisi alisema Charles
No comments:
Post a Comment