Afisa Usalama, Afya Mazingira na
Ubora wa Kampuni ya Asas Cosmas Charles(kushoto) akimkabidhi mganga mkuu
wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa, Alfred Mwakalebela mtambo wa
kisasa wa kutakasa mwili kwa ajili ya hospitali hiyo.
Baadhi ya wananchi wakipita kwenye
mtambo wa kisasa wa kutakasa mwili mzima kwa ajili ya kupambana na
virusi vya corona uliotolewa na kampuni ya Asas ya mkoani Iringa kwa
ajili ya hospitali ya rufaa ya Iringa. (picha na Denis Mlowe)
…………………………………………………………………………………..
NA DENIS MLOWE. IRINGA
KAMPUNI ya Asas imegawa msaada wa
mtambo maalum wa kutakasa mwili na barakoa zaidi ya 1200 kwa ajili ya
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na hospitali za ya wilaya kwa ajili
ya
kujinga na kuenea kwa Virusi Vya Corona.
Msaada huo umekabidhiwa jana
kwa mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa, Alfred
Mwakalebela na Afisa Usalama, Afya Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Asas
Cosmas Charles kwa niaba ya mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni hiyo,
Ahmed Salim Abri sambamba na kutoa msaada wa ndoo maalum za kunawa
mikono 80.
Akizungumza na wanahabari mara
baada ya kukabidhi msaada huo, mwakilishi huyo, Cosmas Charles amesema
kampuni hiyo imeamua kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na
ugonjwa wa corona ambao umekuwa tishio nchini na duniani kwa ujumla.
Alisema kuwa kampuni ya Asas
mkoa wa Iringa imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii hasa katika
suala zima la kupambana kuenea kwa virusi vya corona mkoani hapa na
kuweza kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.
Alisema kuwa kama kampuni
wameitikia maagizo ya serikali kuhusu kuzingatia masuala ya usafi katika
maeneo ya kazi kama sehemu ya kupambana na tishio la maambukizi ya
virusi vya ugonjwa wa corona na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii
wakiwemo madereva bodaboda, umoja wa daladala kwa kuwapatia vifaa
mbalimbali vya kujinga dhidi ya maambukizi ya corona.
Alisema kuwa wametoa msaada
huo ambao mtambo maalum wa kutakasa mwili mzima ambao ni wa kwanza kwa
hospitali za rufaa za nyanda za juu kusini na ya pili nchini kuwana na
mtambo huo hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa jamii na wafanyakazi
wa hospitali hiyo kujikinga dhidi ya maambukizi hayo.
Aidha aliongeza kuwa jamii
inatakiwa kuwa na utamaduni wa kujiweka safi katika mazingira wanayoishi
na hali ya hii ya kunawa mikono kwa sabuni inatakiwa kuwa utamaduni
ambao unafanyika kila siku kuliko kusubiri changamoto kama hizi za
gonjwa la corona.
Cosmas alisema kuwa kampuni ya
Asas ni wadau wakubwa katika masuala ya afya na wadau wa maendeleo kwa
ujumla hivyo msaada huo ni kuhakikisha wananchi wote wanaenda katika
hospitali hiyo wanajikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo
vimekuwa vinahatarisha maisha ya binadamu kote duniani.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa
Hospitali ya Rufaa , Alfred Mwakalebela alisema kuwa msaada umekuja
wakati muafaka katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Corona na
kuwashukuru kampuni ya Asas kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia
sekta ya afya.
Alisema kuwa kampuni hiyo
imekuwa ikisaidia maeneo mbalimbali katika hospitali hiyo ikiwemo ujenzi
wa wodi ya watoto, nyumba ya damu salama, ujenzi wa ICU ya kisasa
pamoja na mashine zake ununuzi wa Xlay ya kisasa na bila kuchoka wametoa
mtambo bora kabisa wa kutakasa mwili mzima.
Alisema kuwa kampuni hiyo
imefanikiwa kujenga karakana ya kutengeneza viungo bandia vya miguu na
mikono ambayo inatarajia kuanza kufanya kazi hivi karibuni hali ambayo
imesaidia kwa kiasi kubwa kuifanya sekta ya afya kujivunia uwepo wake.
Mwakalebela alisema kuwa
kampuni hiyo imefanikiwa pia kuwapatia ndoo maalum za kunawa mikono 80
ambazo watazitumia kuzigawa kwa vituo vya vya afya na hospitali za
wilaya na kuahidi kuvitumia vyema na kuwapa elimu zaidi wananchi
wanaokwenda kupata huduma hospitali.
“Kwa kweli kampuni ya Asas
imekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi mkoani Iringa na kikubwa zaidi
sekta ya afya kwani wameweza kuitendea haki kwa kweli na kuwataka wadau
wengine kujitoa kama ambavyo kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele
kujitoa kwa jamii.
No comments:
Post a Comment