Pages

Friday, May 1, 2020

MZEE WA MIAKA 75 ASHITAKIWA KWA RC KWA KUIBA MKE WA MTU



……………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -PEMBA.
MZEE Haroub Ali Kombo miaka 75 mkazi wa kisiwa cha  Fundo Mkoa wa Kaskazini Pemba amefikishwa ofisini kwa mkuu wa mkoa huo baada ya kushitakiwa na mzee mwenzake
mwenye umri sawa  (jina linahifadhiwa) akimlalamikia kwamba anamchukulia mke wake.
Hii ni mara ya pili wazee hao kufikishana mbele ya serikali  ya Mkoa kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu sasa.
Akitoa maelezo yake , malalamikaji(jina tunalo)alisema mzee mwenzake ameshindwa kuheshimu makubaliano ya awali na bado anaendelea na tabia yake.
Alieleza kwamba pamoja na makubaliano ya awali yaliyofanyika mbele ya uongozi wa Mkoa, ameshindwa kuyatekeleza naumia sana.
“Inauma sana kuona mke wangu anachukuliwa na mzee mwenzangu , naomba Mhe Mkuu wa Mkoa unisaidia ili tuikomesha tabia hii”alisema.
Katika maelezo yake , Haroub Ali Kombo alisema amechoshwa na maneno  hayo na kwamba anajiandaa kuhama kisiwani humo na kurudi kwao Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.
“Kwa kuwa limenitokea mimi naonekana mkorofi, hivyo mhe Mkuu wa Mkoa namuomba sheha aende kusimamia kuuza mazao yangu ili nirudi nilikotoka Kiwani”alieleza.
Alisema tangu walipoitwa kwa mara ya kwanza yeye alikata mawasiliano na mwanamke huyo hata vipndo walivyokuwa wakilima pamoja waligawana.
Sheha wa shehia ya Fundo Khamis Abeid alikiri kuendelea mawasiliano kati ya mzee huyo na mwanemke huyo licha ya hapo awali wawili hao kutakiwa kukatisha mahusiano.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete Kepteni Khatib Khamis Mwadini alitaka sheria zaa kinidhamu zichukuliwe kwa mze huyo kwani ameshindwa kuheshimu maamuzi yake mwenyewe.
“Kikao kilichopita mzee huyu aliahidi kwamba anaenda kuhamisha mali zake ili arudi alikotoka , lakini kumbe alikuwa anafanya utani , lazima alazishw kushehimu maamuzi yake”alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman alisema serikali haiwezi kuchezewa hivyo mzee huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kali.
Alisema awali mzee Haroub kwa kinywa chake alitamka kuvunja mahusiano na mke wa mtu na kutaka mashamba na vipando walivyolima pamoja vigawanywe ili kila mmoja ili mawasiliano yasiwepo.
“Mwenye mke analalamika kwamba bado unaendelea na mahusiano na mke wake, hivyo serikali inachokihofia na kutokea ambayo hayakutarajiwa”alisema.
Hata hivyo kwa mara nyengine Mzee Haroub aliomba serikali isimchukulie hatua kali kwani , alimtaka Sheha wa shehia hiyo kumtafutia wateja kwa ajili ya kuuza mazao yake .

No comments:

Post a Comment