Pages

Friday, May 1, 2020

MATUKIO KATIKA PICHA KUAGWA KWA MWILI WA MAREHEMU JAJI RAMADAHANI



Mke wa aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Marehemu  Augustino Ramadhani,  Saada Ramadhani (katikati)  ambaye  ni Luteni Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi  wa Tanzania (JWTZ) akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe leo kwenye viwanja vya Karimjee vilivyoko Jijini Dar es Salaam wakati wa   Mazishi ya Kitaifa.
Watoto wa  aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Marehemu  Augustino Ramadhani na ndugu wakimsaidia Mke wa marehemu, Saada Ramadhani (katikati)  ambaye  ni Luteni Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi  wa Tanzania (JWTZ) kwenda kwenye gari kwa ajili ya kuondoka kwenye viwanja vya Karimjee vilivyoko Jijini Dar es Salaama  leo mara baada ya  Mazishi ya Kitaifa kumalizika. 
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa (kushoto) na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Nne, Mhe. Jakaya Kikwete (kulia), wakiwemo Majaji Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Mhe. Barnabas Samatta na Mhe. Mohamed Chande Othuman wakiwa katika Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Marehemu Augustino Ramadhani, yaliyofanyika leo viwanja vya Karimjee vilivyoko Jijini Dar es Salaam.
Gari lililokuwa limebeba  jeneza la   mwili wa aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Marehemu  Augustino Ramadhani likiingia katika viwanja vya Karimjee vilivyoko Jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya Mazishi ya Kitaifa  Mazishi ya Kitaifa.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa katika Mazishi hayo.

Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Tatu, Mhe. Benjamin, Mama Anna Mkapa (kulia) na Mke Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Nne, Mama Salma Kikwete (katikati), na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Damian Lubuva (kushoto) wakiwa wamesimama mara baada ya jeneza la   mwili wa aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Marehemu Augustino Ramadhani kuingia katika viwanja vya Karimjee vilivyoko Jijini Dar es Salaam wakati wa   Mazishi ya Kitaifa yaliyofanyika leo.
Baadhi ya viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wadini wakiwa katika Mazishi hayo.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa   mwili wa marehemu.
Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Tatu, Mama Anna Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu Nne, Mhe. Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa pole kwa familia ya marehemu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa   heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Jaji Mkuu   Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Barnabas Samatta akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othuman akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Picha na Magreth Kinabo- Mahakama.

No comments:

Post a Comment