Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir
Saleh akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho ili
kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinavyoendelea kiwandani
hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari na
maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakielekea katika eneo la uzalishaji wa
Trasfoma wakati walipotembelea kiwanda cha Tanalec Limited cha jijini
Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na kazi ya uzalishaji wa Trasfoma.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir
Saleh akiwapa maelezo waandishi wa habari namna uzalishaji wa Trasfoma
unavyoendelea walipotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli
mbalimbali za uzalishaji zinavyoendelea.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir
Saleh akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya Transfoma ambazo ziko
katika hatua mbalimbali za utengenezaji wakati waliotembelea kiwanda
hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji zinavyoendelea.
…………………………………………………..
Soko la Trasfoma kwa Tanzania
nikubwa sana ukilinganisha na kipindi kiingine ambapo kwa
mwaka uliopita
tumeuza Transfoma 8000 huku mradi wa umene vijijini peke yake
wakichukua Transfoma 300.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir
Saleh ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli mbalimbali za
uzalishaji zinavyoendelea kiwandani hapo.
Bw. Zahir amesema soko la
Tanzania ni kubwa na wao wanakidhi haja ya soko kwa sababu uzalishaji wa
Transfoma na vifaa mbalimbali unaenda vizuri na kwa kiwango cha hali ya
juu.
“Nalipongeza shirika la umeme
nchini TANESCO kwa kudhibiti tatizo la kukatikakatika kwa umeme na
kuzalisha umeme wa kiwango kizuri na wakutosha, hili limetufanya
kuendelea vizuri na uzaishaji wa bidhaa kiwandani hapa”.
Umeme kwa sasa kukatika imekuwa
ni historia inaweza kupita hata miezi mitano ukakatika mara moja na
baada ya muda mfupi unarudi kwa kweli kwa hili nawapongeza TANESCO”
Amesema Bw. Zahir Saleh.
Amesema kwa sasa wanayo masoko
mengine katika nchi nyingi za Afrika kama vile Kenya, Uganda, Rwanda,
Zambia, Ethiopia na nyingine.
Amesema lengo kiwanda hicho ni
kuzifikia nchi nyingi za Afrika ili kupanua soko zaidi huku akitolea
mfano wa Kenya ambayo imewapa tenda ya Dola Milioni sita ili kuwauzia
Transfoma.
No comments:
Post a Comment