Bw. Bernrad Dadi Mkurugenzi wa
Mfumo wa Malipo wa Taifa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) aktoa mada kuhusu
Kanzidata ya Kudumu ya Watoa Huduma za Kifedha Financial Services
Register (FSR) katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha
leo.
Bw. Augustine Hotay Mkurugenzi wa
Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akitoa mada kuhusu
matumizi safi ya Noti na utambuzi wa alama muhimu zilizopo katika Noti.
Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akizungumza na washiriki wa semina ya Uchumi na Fedha inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari
wanaoshiriki katika semina hiyo wakiangalia alama muhimu zilizopo kwenye
Noti ya Shilingi elfu 10.000.
………………………………………..
Benki Kuu ya Tanzania BoT
imeanzisha mfumo mpya wa huduma za kifedha kwa
kushirikiana na wadau
wengine ambao ni CDC, TIRA TCDC CMSA na TAMISEMI ili kutengeneza
Kanzitada itakayowaorodhesha watoa huduma wote wa shughuli za Kifedha.
Bw. Bernrad Dadi Mkurugenzi wa
Mfumo wa Malipo wa Taifa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) amesema hayo mara
baada ya kutoa mada kuhusu Kanzidata ya Kudumu ya Watoa Huduma za
Kifedha Financial Services Register (FSR) katika semina ya waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari inayoendelea kwenye tawi
la BoT jijini Arusha leo.
Amesema hapo mwanzo BoT ilikuwa
ikipata taarifa au data kwa kutumia tafiti ambazo zilikuja kuonekana
zina mapungufu kwasababu zilikuwa zinachukua muda kupatikana lakini
pia ilikuwa ni gharama kubwa kwa sababu ili kupata hizi data au taarifa
ilibidi kuajili kampuni au kikundi ili kutapita nchi nzima ili kukusanya
taarifa hizo.
Amesema Mwaka 2012 na 2014, tafiti mbili za kijiografia za maeneo ambayo huduma za kifedha
hupatikana zilifanyika Tanzania na FSDT kwa niaba ya Benki kuu ya Tanzania, ukiangalia hapo utagundua ni kipindi cha mwaka mzima ulipita hivyo utaona hapa katikati kulikuwa na watoa huduma ambao hawakusajiliwa.
hupatikana zilifanyika Tanzania na FSDT kwa niaba ya Benki kuu ya Tanzania, ukiangalia hapo utagundua ni kipindi cha mwaka mzima ulipita hivyo utaona hapa katikati kulikuwa na watoa huduma ambao hawakusajiliwa.
Ameongeza kuwa jambo lingine
lilikuwa ni kwamba taarifa hizi ziko maeneo mbalimbali, Kwa mfano ili
kujua mawakala wa bima ilibidi lazima uende TIRA kupata taarifa zao,
Ili kujua mawakala kampuni za simu ilibidi kwenda Tigo, Vodacom,
Airtel na kadhalika na ukitaka kupata taarifa za SACCOS ilibidi pia
uende kwenye SACCOS zao , hivyo ilikuwa vigumu sana kupata taarifa
sahihi.
Bw. Bernrad Dadi amesema hili
ndilo lililofanya wasimamizi wa huduma za fedha BoT na wadau wengine
kama CDC, TIRA TCDC CMSA na TAMISEMI kukaa pamoja na kutengeneza
Kanzitada hiyo ambayo iitatupa faida Watunga sera kujua wapi huduma
hazijafika, Wawekezaji kujua wapi hawapo hapa nchini ili kujipanga
kupeleka huduma sehemu ambazo hawapo. Lakini pia kuwajua watoa huduma
za kifedha wakubwa na wadogo popote walipo na shughuli wanazofanya.
“Wasimamiiaji wa huduma hizi
hatuna tena sababu ya kwenda Tigo , Halotel, Vodacom na maeneo mengine
ili kujua ana mawakala wangapi, taarifa hizo tutakuwa tunazipata kwa
pamoja na kuzitoa kwa pamoja . pia itasaidia katika utekelezaji wa Sera
za nchi ambazo tunaita (National Financial Inclussion Framework)
ambazo zinatekelezwa”. Amesema Bw. Dadi.
Ameongeza kuwa utengenezaji au
uundaji wa Kanzidata yenyewe umeshakamilika kwa asilimia 98 yamebaki
mambo ya taarifa mbayo watumiaji watatuambia na kushauri namna ya
kuziweka taarifa hizo.
Usajili wa watoa huduma hao
awamu ya kwanza utaanza mwezi huu wa Machi na Aprili ambapo na awamu
ya pili ya usajili huo itafanyika mwezi Mei na Juni mwaka huu.
Ameongeza kuwa itakapofika Julai
Mosi mwaka huu mfumo huu utakuwa uko tayari na una taarifa zote , baada
ya hapo wataachiwa watoa huduma wakubwa ambao wataendelea kuwasajili
watoa huduma wapya kadiri watakavyoandikisha, baada ya hapo tutakuwa
tunawajua watoa huduma wote wakubwa na wadogo nchini.
Amesema ukishawaunganisha watoa
huduma hao na mifumo mingine kama vile Tanzania InteBank Payment System
(TIPS) utakuwa na uwezo wa kujua hela hizi zimetoka mkoa huu na kwenda
mkoa huu na kwa kutumia Kanzidata hii tutajua na kupata takwimu
sahihi za miamala ya fedha iliyofanyika na kuleta ufanisi wa huduma za
kifedha nchini .
No comments:
Post a Comment