……………………………………………………………………………………….
Na Farida Saidy,Morogoro
Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muunano wa Tanzania Mhe. Kasimu
Majaliwa ameeleza kusikitishwa na kitendo cha wakala wa Barabara Nchini
(TANROAD) kushindwa kurejesha...
mawasiliano ya barabara ya Morogoro –
Dodoma kwa siku tatu sasa, huku akisema kitendo hicho ni uzembe na
kulizalilisha taifa ukizingatia Barabara hiyo ni Kiungo kati ya Tanzania
na Mataifa mbalimbali.
Mpaka Leo March 4,2020 Ni siku ya
tatu sasa tangu kukosekana kwa mawasiliano ya barabara katika eneo hilo
la Kiyegeya, na hii ni baada ya Daraja la mto Mkange kusombwa na
maji,ambapo kwa Sasa abiria pekee ndio wakilazimika kuvuka upande wa
pili kwa miguu kutafuta usafiri mbadala baada ya Magari makubwa ya
Abiria nay ale ya mizigo kushindwa kupita.
Toka Jumatatu March 2, majira ya
saa 10 jioni iliporipotiwa Daraja hilo kusomwa na Maji,huku jitihada
mbalimbali zimefanyika kurejesha mawasiliano,Na viongozi mbalimbali
wakilazimika kukesha eneo la tukio lakin inaonekana Hali kuwa bado si
swari.
Hata hivyo Waziri mkuu Kassim
Majaliwa amefika kujionea hali halisi katika eneo Hilo ambapo amesema
kitendo Cha TANROAD kushindwa kurejesha Barabara hiyo ni uzembe wa Hali
ya juu.
Aidha amemtaka waziri mwenye
dhamana ya ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano, kuongeza usimamizi kwa kuomba
nguvu ya ziada toka jeshi la wananchi pamoja na Timu ya wataalam wa
Ujenzi kutoka Mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Waathirika wakubwa ni Madereva wa
Mabasi na Magari mengine ya Mizigo, wanaasema pamoja na kuahidiwa Daraja
hilo lingekamilika mapema hadi sasa wanaendelea kuishi kwa shida
ukizingatia eneo lenyewe hakuna huduma za kijamii.
Pamoja na mambo mengine waziri
mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi huo kufanyika usiku na mchana
kuwezesha ndani ya saa 24 mawasiliano yanarejee kuwezesha shughuli za
kiuchumi kuendelea.
No comments:
Post a Comment