…………………………………………………………………………………………….
*Ni baada ya kushindwa kukagua madaraja kwenye eneo lake
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROAD), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe
wizarani na nafasi yake ijazwe na...
mtu mwingine mara moja baada ya
kuzembea kutimiza wajibu wake.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya lililopo eneo la
Gairo ambalo limesombwa na maji na kusababisha kukatika kwa
mawasiliano kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020. Wa pili kulia ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya lililopo eno la Gairo
ambalo limesombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya
barabara kati ya Morogoro na Dar es salaam, Machi 4, 2020. Kushoto ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya lililopo eneo la
Gairo ambalo llimesombwa na maji na kusababisha kukatika kwa
mawasiliano ya barabara ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi
4, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipita kwenye msururu wa magari yaliyokwama baada ya daraja la
Kiyegeya kusombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya
barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapa pole baadhi ya madreva na abiria waliokwama baada ya daraja la
Kiyegeya kusombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya
barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020.
Eneo la daraja la Kiyegeya ambalo
lilisombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara
kati ya Morogoro na Dodoma , ukarabati wake unaendelea. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Pia, Waziri Mkuu
ametoa onyo kwa Mameneja wa TANROAD wa mikoa yote nchini waache kukaa
maofisini na badala yake wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ipasavyo
ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa madaraja yote ili
kujiridhisha na hali ya usalama hususani katika kipindi hiki cha mvua.
Uamuzi huo
umekuja baada ya kiongozi huyo kushindwa kufanya ukaguzi wa usala wa
madaraja yaliyoko kwenye mkoa wake na kubaini kama kuna daraja
linamatatizo hali iliyosababisha daraja la Kiyegeya lililopo wilayani
Kilosa ambalo linaunganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kuvunjika.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo(Jumatano, Machi 4, 2020) baada ya kutembelea eneo
hilo na kukagua ukarabati ili kurejesha mawasiliano ya barabara. Waziri
Mkuu ameshuhudia mrundikano wa magari na abiria hali ambayo
haikumfurahisha.
“Hivi unajua
udhahifu wako ni kwa sababu hukufanya ukaguzi kuona kama daraja limejaa
mchanga au uchafu ambao umesababisha kipenyo cha kupitisha maji kuwa
kidogo na maji yakalazimika kupanda juu hali ambayo ilisababisha daraja
hili kusombwa na maji.”
Amesema wakati
njia hiyo inarekebishwa itengenezwe njia nyingine ya muda ili kuweza
kupitisha magari na kisha Serikali itachukua hatua baada ya kubaini nini
kimesababisha.
Ili kuharakisha
kazi hiyo inakamilika kwa haraka, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara
hiyo pamoja na wahandisi wote wa TANROAD mkoa wa Morogoro na Dodoma leo
wakutane kwenye eneo la tukio na wahakikishe kuanzia kesho (Alhamisi,
Machi 5, 2020) njia hiyo iwe imefunguka.
Kadhalika, Waziri
Mkuu amesema atawasiliana na Mkuu wa Majeshi, Generali Venance Mabeyo
ili aweze kupata msaada wa wanajeshi ili waongeze nguvu katika
kuhakikisha kwamba mawasialaino yanarejea kwa haraka.
Akiwapa pole
madereva na watumiaji wengine wa barabara waliokwama katika eneo hilo,
Waziri Mkuu amesema “Nimetumwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuja
kuwapa pole na kuwahakikisha kwamba Serikali inafanya kila
linalowezekana ili kuifungua barabara hii.”
No comments:
Post a Comment