Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akisikiliza taarifa
ya msitu wa asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye
ekari 12.3 kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza, Salim Ali (kulia) alipofanya ziara wilayani humo. Kushoto ni
Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Kipole na wa pili kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya hiyo, Magesa Mafuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia msitu wa
asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye ekari 12.3
uliopomeneo la makamu makuu ya Halmashauri hya wilaya ya Sengerema ambao
unatumika kama shamba darasa kwa wananchi kuhusu uhifadhi endelevu wa
mkisitu yua asili katika maeneo hayo ambao kwa mujibu wa Afisa Mazingira
wa Wilaya ya Sengerema Salim Ali, utasaidia kunyonya hewa chafu,
upatikakaji wa kuni kupitia uvunaji maalumu na uwekaji wa shughuli
rafiki wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akipanda mti na
mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani wilayani Sengerema mkoani
Mwanza alipofanya ziara ambapo pia alizungumza na wanafunzi wa shule
hiyo kuhusu utunzaji mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitembelea na
kukagua kikundi cha mazingira Bwawani wilayani Sengerema mkoani Mwanza
ambapo aliwapongeza na kuwatangaza kuwa mabalozi wa Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na
wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani ambapo aliwataka wawe mstari wa
mbele katika utunzaji wa mazingira.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
No comments:
Post a Comment