……………………………………………………………………..
Na Farida Saidy, Morogoro
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema daraja la Mto Mkange
lililopo Wilayani Kilosa lililovunjilka Machi 2 mwaka huu, linatarajiwa
kukamilika usiku wa kuamkia Machi 4 mwaka huu.
Waziri Kamwelwe amesema hayo akiwa
katika eneo la tukio, mara baada ya
Karavati moja kati ya mawili
yanayohitajika kushushwa sehemum lilipokatika daraja na kutoa matumaini
kuwa ujenzi wa daraja hilo la muda utakamilika usiku wa kuamkia Machi 4
Mwaka huu.
Hata hivyo Waziri amesema kuwa
daraja hilo kwa sasa halitapitisha magari mawili kwa pamoja badala yake
gari moja tu litaruhusiwa kupita hadi hapo utaratibu mwingine
utatakapotolewa.
Aidha, Waziri amesema karavati la
awali ambalo limevunjika lilikuwa na kipenyo cha Mita tatu tu na sasa
yamewekwa makaravati mawili kila moja likiwa na kipenyo cha Mita tatu
hivyo kuruhusu maji mengi kupita kwa wakati mmoja tofauti na awali.
Akitoa matumaini kwa watanzania
hususana madereva wanaotumia barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, Waziri
amesema kazi ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo utafanyika
mara baada ya mvua kupungua.
Kwa upande waka Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Loata Ole Sanare amewashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa
waliouonesha tangu adha hiyo ilipotokea hususan madereva kwa kutii
maelekezo ya Serikali walipotakiwa kubaki maeneo waliyokuwapo hadi
watakapoelekezwa vingine.
Daraja la Mto Mkange lililopo
katika Kijiji cha Kiegeya Wilayani Kilosa lilivunjika Machi 2 Mwaka huu
majira ya saa kumi jioni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
hapa nchini na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na Usafirishaji.
No comments:
Post a Comment