Kamishina wa Mafuta
na Gesi kutoka Wazira ya Nishati, Bw.Adam Zuberi akiendesha Mkutano wa
Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika Leo katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Tanzania.
Mkurugenzi wa
Miundombinu Sekritarieti ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Mapolao Rosemary Makoena akiwa
kwenye Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka nchi wanachama ulimalizika
leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wataalam wa Sekta
ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia mkutano huo uliomalizika leo leo
Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwakilishi kutoka
Angola akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC
uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwakilishi kutoka
Msumbiji akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC
uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwakilishi kutoka Tanzania
akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC
uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)
Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Picha Idara ya Habari-MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
KAMATI ya Wataalamu wa Nishati
katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
imependekeza mataifa hayo kuwa na sheria rasmi za kusimamia miradi ya
kimkakati
katika sekta ya nishati ili kuwa na utoshelevu wa uhakika wa
nishati ya umeme kwa ajili mahitaji ya wananchi wake.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa
(Februari 28,2020) Jijini Dar es Salaama na Kamishna wa Petroli na Gesi
katika Wizara ya Nishati,Adam Zuberi wakati akifunga mkutano wa siku nne
wa Kamati ya Wataalamu wa Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichoanza tarehe 24-28 Februari
mwaka huu.
Alisema katika kikao hicho,
wajumbe hao walitoa mapendekezo mbalimbali yanayotarajiwa kujadiliwa kwa
pamoja katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo
kinachotarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu, ambapo moja ya
mapendekezo yaliyokubaliwa na wataalamu hao ni pamoja na kuweka sheria
rasmi ya kusimamia taasisi za kimkakati katika sekta ya nishati ndani
ya SADC.
‘’Katika SADC tuna miradi mikubwa
ya kimkakati ambayo sasa tumekubaliana iende mbele zaidi kwa Mawaziri
ikiwemo kusaini MOU (mkataba wa makubaliano) ili kuwezesha utekelezaji
wa miradi hiyo inaweza kufanya kazi’’ alisema Zuberi.
Aliongeza kuwa miongoni mwa miradi
ya kimkakati inayotarajiwa kupewa kipaumbele katika uendelezaji wake ni
pamoja na Uimarishaji wa Kituo cha Umahiri katika Uendelezaji wa
Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati (SACREEE) pamoja na
kuratibu utoaji wa mafunzo kwa wataalamu kuhusu nishati ya umeme.
Alibainisha mradi mwingine ni
pamoja na uendelezaji wa kituo cha umahiri cha kafue uliopo nchini
Zambia, ambacho kitatumika kama chombo rasmi cha Jumuiya hiyo
kitakachotumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya
nishati katika jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa Zuberi alisema
mapendekezo mengine yaliyojadiliwa kwa mapana na wataalamu hao SADC ni
makubaliano ya pamoja katika kuwa na miradi ya pamoja ya kimkakati
kuunganisha nchi moja na nyingine ili kuhakikisha kuwa nchi za SADC
zinakuwa na nishati ya umeme wa uhakika.
Kwa mujibu wa Zuberi alisema
mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na kuwa na mpango kabambe wa
matumizi ya gesi asilia (2012-2027)ambapo kwa sasa tayari mshauri
mwelekezi tayari amepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo mwezi Agosti mwaka jana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Miundmbinu wa SADC Bi. Rosemary Makoena alisema katika kikao hicho
wataalamu hao walijikita katika kujadili namna bora ya kusimamia
matumizi ya nishati mbadala ili kuweka kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme
kwa kutosheleza kiwango cha mahitaji ya nishati ya umeme katika SADC.
No comments:
Post a Comment