Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainabu Chaula.
……………………………………………….
Na. Catherine Sungura-Dodoma.
Tanzania ni moja ya nchi mbili afrika zinazofanya vizuri katika kupunguza maambukizi,kutibu pamoja na kupona ugonjwa wa kifua kikuu “TB” na hivyo kufikia asilimia
75 ya malengo yaliyowekwa.Tanzania ni moja ya nchi mbili afrika zinazofanya vizuri katika kupunguza maambukizi,kutibu pamoja na kupona ugonjwa wa kifua kikuu “TB” na hivyo kufikia asilimia
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainabu Chaula wakati wa mkutano wa kupokea ripoti ya tathimini ya mapitio ya mpango mkakati wa kifua na ukoma uliofanyika jijini hapa.
“Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuja kufanya tathimini kwa kushirikia na wataalam wengine kutoka nje na ndani ikiwa ni kuona jinsi gani tumeyafikia malengo tuliyojiweke kwenye mpango mkakati wetu wa mwaka 2015 ikiwemo kuongeza kasi ya kuwafikia wagonjwa kwa asilimia 29 zaidi”.
Amesema kuwa tathimini hiyo ilikua ikiangalia malengo ya kidunia ya kumaliza tatizo la Tb pamoja na ukoma,“asilimia nyingine tumepewa malezo na tutaenda kuyaweka kwenye mpango mkakati mwingine tunaoenda kuuandaa na kuweza kushughulikia”.Aliongeza Dkt. Chaula
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wananchi kwani ugonjwa wa TB unaenezwa kwa hewa hivyo alishauri wananchi kuepuka misongamano,kulala kwenye nyumba zenye madirisha yenye hewa , kuzingatia usafi wa mazingira na kwa watu wenye dalili ni vyema kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata matibabu kwani huduma za TB zinapatikana kuanzia ngazi za zahanati.
Naye Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti na kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) Dkt. Zuweina Kondo amesema kuwa wamefanikiwa kugundua wagonjwa kutoka asilimia 37 mwaka 2015 hadi asilimia 53 hivi sasa.
“Tulikua tumeweka mkakati wa kuwafikia wagonjwa na tumefikia kwa asilimia 43 zaidi kwa mwaka 2018 tuliwafikia wagonjwa 75545 na mwaka 2019 tuliwafikia wagonjwa 82140 , kadri unavyogundua wagonjwa wengi ndio utastopisha yale maambukizi”
Kwa upande wa watoto Dkt. Zuweina amesema kuwa wameweza kufikia lengo la WHO kwa asilimia 15 ambalo ni lengo la juu lililotajwa kidunia ambapo Tanzania ni kati ya nchi saba ambazo zipo katika kufikia malengo ya kidunia ya mwaka 2020 ya kupunguza maambukizi mapya kwa kila mwaka kwa asilima nne (4) ukilinganisha na asilimia mbili (4) kwa nchi nyingine ambazo ni kiwango cha kawaida.
Dkt. Zuweina amesema kwa upande wa ukoma hivi sasa wameweza kuondoa ugonjwa huu kutoka halmashauri za wilaya 19 mwaka 2015 kubakiza halmashauri 16 hivyo wanajipanga kuondoa kwenye halmashauri zilizobaki kwa kuendeleza kutoa elimu na kutafuta njia nyingine za kuwafikia wagonjwa.
No comments:
Post a Comment