Pages

Friday, February 28, 2020

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA APOKEA UJUMBE KUTOKA SEKRETARIETI YA SOKO LA PAMOJA LA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA COMESA




Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Ludovick Nduhiye wakiwa katiza picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Sekretarieti ya COMESA ulioongozwa na Balozi Dr. Kipyego Cheluget.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia miradi kutoka sekretarieti ya (COMESA) Balozi Dr. Kipyego Cheluget.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akiongoza kikao kujadili utekelezaji wa mradi wa uwezeshaji biashara (Trade Facilitation) na kuimarisha biashara ya mipakani (Cross Border Trade).
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akisisitiza jambo kwa na Balozi Dr. Kipyego Cheluget ambaye ni Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia miradi kutoka sekretarieti ya (COMESA) kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Ndugu Ludovick Nduhiye katika ofisi za wizara Mtumba, jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 27 Februari, 2020 amepokea ujumbe kutoka Sekretarieti ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa
Afrika (COMESA) ulioongozwa na Balozi Dr.Kipyego Cheluget, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miradi.
Ujumbe huo ulifika katika ofisi za wizara zilizopo katika eneo la Mtumba jijini Dodoma lengo likiwa ni kukutana na Menejimenti ya Wizara kuzungumzia utekelezaji wa mradi unaohusu uwezeshaji biashara (Trade Facilitation) na kuimarisha biashara ya mipakani (Cross Border Trade).
Pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajia kuchochea na kurahisisha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya za COMESA, EAC na SADC.

No comments:

Post a Comment