Katibu wa chama cha mapinduzi ccm
bi zubeda abdalah akiwasisitiza wananchi watoke nje ili kuokoa maisha
yao dhidi ya mafuriko ambayo yametokea karibu na shule ya msingi
sombetini picha na Queen lema Arusha.
*************************************
Na Queen Lema Arusha
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida mvua zinaziendelea kunyesha jijini arusha zimesababisha maji
kujaa katika shule ya msingi sombetini hali ambayo imesababisha viongozi
mbalimbali wa
chama cha mapinduzi kutoa maji hayo
Akizungumza ndani ya
shule hiyo ya sombetini katibu wa Uwt kata ya sombetini Bi Mwajaby
Mvamba amesema kuwa mvua hizo zilianza kunyesha majira ya saa tisa na
imeharibu miundombinu ya shule hiyo
Alisema kuwa wao kama
viongozi wa chama wamelazimika kutoa maji ambayo yameharibu vibaya
miundombinu ya shule hiyo ambayo wanafunnzi wanatarajia kufungua shule
january 6 mwaka huu
“Maji ni mengi sana kwa
kweli yamejaa sana na hata huenda hata taarifa mbalimbali zikaharibika
ila tunapambana sana kuhakkisha madhara hayatokei kwa maslahi ya shule
yetu”
Naye katibu wa Osunyai
jr Zubeda Abdalah alisema kuwa wao kama wadau wa elimu wanaomba serikali
kuboresha miunfombinu zaidi ya shule hasa hiyo ya sombetini
Zubeda alifafanua kuwa
kwa masaa machache wamelazimika kuarisha kazi zao na kutoa maji ambayo
yalikuws yamejaa katika shule hiyo ya sombetini na madarasa ambayo
yamedhurika na maji hayo ni madarasa ya awali darasa la kwanza na darasa
la pili.
No comments:
Post a Comment