Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina,akizungumza katika kikao cha wadau kujadili namna ya kunusuru
Machinjio ya Dodoma kilichofanyika katika ofisi za Kampuni ya TMCL.
Kaimu Meneja wa machinjio ya
Dodoma Victor Mwita,akijitambulisha katika kikao cha wadau kujadili
namna ya kunusuru Machinjio ya Dodoma kilichofanyika katika ofisi za
Kampuni ya TMCL.
Sehemu ya washiriki na waandishi
wa habari wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhanga
Mpina katika kikao cha wadau kujadili namna ya kunusuru Machinjio ya
Dodoma kilichofanyika katika ofisi za Kampuni ya TMCL.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko
Bw.Felix Nandonde,akizungumza katika kikao cha wadau kujadili namna ya
kunusuru Machinjio ya Dodoma kilichofanyika katika ofisi za Kampuni ya
TMCL.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina,akisisitiza jambo katika kikao cha wadau kujadili namna ya
kunusuru Machinjio ya Dodoma kilichofanyika katika ofisi za Kampuni ya
TMCL.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………
Na Alex Sonna,Dodoma
Serikali imevunja mkataba wa mauzo ya mali za machinjio ya Dodoma(TMCL) baina yake na kampuni ya NICOL uliosainiwa mwaka 2008 huku ikiitaka kampuni hiyo kulipa zaidi ya
Sh.Bilioni 14.96 za madeni ya TMCL
na mapunjo katika biashara ya machinjio kwa serikali.Na Alex Sonna,Dodoma
Serikali imevunja mkataba wa mauzo ya mali za machinjio ya Dodoma(TMCL) baina yake na kampuni ya NICOL uliosainiwa mwaka 2008 huku ikiitaka kampuni hiyo kulipa zaidi ya
Sambamba na hilo, Vyombo vya ulinzi na usalama vimeagizwa
kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wote wa NICOL, NARCO na TMCL
waliohusika na ubadhirifu wa mali za TMCL na kuisababishia hasara
serikali tangu mwaka 2008.
Hatua hiyo imefikiwa leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina katika kikao cha wadau kujadili namna ya kunusuru machinjio hiyo.
Mpina amesema mkataba huo umevunjwa kwa kuzingatia Ibara ya 7 na
13 ya mkataba wa mauzo ya mali na hivyo kuanzia sasa machinjio hiyo
itakuwa chini ya serikali.
“NICOL ilipe serikali Sh.9,712,127,660 ambazo serikali ilipunjwa
katika biashara ya machinjio na pia NICOL ilipe madeni yote inayodaiwa
kampuni ya ubia TMCL kiasi cha Sh.5,248,084,000,”amesema.
Aidha, ameitaka kampuni ya NARCO ijiondoe katika Kampuni ya Ubia TMCL ndani ya siku 60 kuanzia leo.
“Huduma za uchinjaji zitaendelea kutolewa kama kawaida katika
kipindi cha mpito chini ya usimamizi wa serikali wakati mchakato wa
kumpata mwekezaji mahiri wa mpito na wa kudumu unaendelea,”ameeleza.
Mpina amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
Dk.John Magufuli ambayo imejipambanua kuwa serikali ya viwanda na
wanyonge haitakubali hujuma na ufisadi uliokuwa ukifanyika katika
machinjio hayo kuendelea.
“Aidha, nataka niwahakikishie kuwa waliohusika na wizi na
ubadhirifu hawatapona, tunajua kuwa hata mishahara ya wafanyakazi nayo
ilifanyiwa ufisadi na kuleta usumbufu mkubwa, pia tunatambua mahitaji ya
uchinjaji mifugo na kusafirisha nyama nje ya nchi ambapo kusimama kwa
machinjio hii kulisababisha wafugaji na vijana wengi kukosa ajira na
masoko ya uhakika,”amesema.
Amewaomba wadau wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na
uendeshaji wa machinjio hiyo waipe muda serikali kushughulikia
changamoto zilizopo.
“Katika kipindi cha muda mfupi machinjio ya Dodoma itafufuliwa na kupanuliwa na kuwa ya kisasa zaidi,”amesema.
Akizungumzia baadhi kasoro zilizobainika, Waziri Mpina amesema
NICOL tangu ikabidhiwe mali hizo kwa kipindi cha miaka 11 haijawahi
kutoa gawio kwa serikali.
Pia amesema nchi imepoteza ajira, fedha za kigeni, biashara na
masoko ya mazao ya mifugo baada ya kiwanda kufungiwa kuuza mazao ya
mifugo katika nchi za Jumuiya ya Kiarabu(UAE).
“Aidha, kampuni 10 zilisimama kusafirisha na kufanya biashara ya
nyama baada ya kiwanda kufungiwa, ambapo kwa mwezi mauzo ya nyama nje
ya nchi katika machinjio yalikuwa yamefikia tani 192 sawa na mbuzi
24,000 kwa mwezi, pia kiwango cha uchinjaji ng’ombe kushuka kutoka
wastani wa ng’ombe 120 hadi 50 kwa siku,”amesema.
No comments:
Post a Comment