Pages

Saturday, December 28, 2019

TEMESA YAKANUSHA UVUMI UNAOENEA MITANDAONI KUSIMAMA KWA HUDUMA ZA VIVUKO KIGONGO BUSISI MKOANI MWANZA



TEMESA inapenda kukanusha uvumi unaoenea mitandaoni kupitia video pamoja na picha zikielezea kusimama kwa huduma za vivuko katika kivuko cha Kigongo Busisi mkoani
Mwanza kutokana na kuwepo kwa magugu maji. Tukio la magugu maji lilitokea siku ya tarehe 24 Desemba 2019 na magugu maji hayo yaliondolewa. 
Shughuli za uvushaji abiria zinaendelea kama kawaida katika kivuko cha Kigongo Busisi. TEMESA inapenda kuwataarifu abiria wote waendelee kutumia huduma za kivuko hicho kwakua kipo salama 
Aidha TEMESA inawakumbusha abiria wote kuzingatia matangazo ya usalama yanayotolewa na mabaharia watumiapo vivuko. 
Imetolewa na Kitengo cha Masoko Habari na Uhusiano kwa Umma TEMESA 

No comments:

Post a Comment