Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akimkabidhi vitendea kazzi Injinia
Emmanuel Koroso Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege
la (ATCL) wakati alipoizindua rasmi bodi hiyo itakayofanya kazi kwa
miaka mitatu mingine katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Shirika
hilo mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam.
………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Ndege la ATCL kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa akipindi cha
miaka mitatu iliyopita.
Waziri Kamwelwe ameyasema hayo
wakati akizindua bodi hiyo baada ya Mwenyekiti wake Injinia Emmanuel
Koroso na wajumbe wake kuteuliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka
mitatu.
Waziri Kamwelwe amesema tulianza
tukiwa na kandege kamoja tu lakini kwa muda wa miaka minne tayari tuna
ndege 7 na nyingene ya 8 itawasili wakati wowote kwa kweli mmefanya kazi
nzuri katika kipindi hicho.
“Changamoto lazima ziwepo lakini
mmefanya kazi nzuri ya usimamizi na msiniogope nikipiga simu nataka
tuwasiliane tuelewane kutatua changamoto hizo ili twende sawa” Amesema
Kamwelwe.
Ameongeza kwamba uwekezaji katika
shirika la ndege la (ATCL) ni Mkubwa sana hivyo mmeaminiwa kusimamia
uwekezaji huo ambao ni fedha za watanzania wanyonge hivyo mkaendelee
kuzisimamia vizuri ili kuwaletea mafanikio watanzania.
Kuteuliwa kwenu tena kuwa katika
Bodi ya wakurugenzi ya (ATCL) ni wazi kwamba mmeaminiwa hivyo mkafanye
kazi kwa weledi na kulisimamia vizuri shirika ili liweze kukua na
kuingia kwenye ushindani wa biashara ya usafiri wa anga.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano
na Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akimkabidhi vitendea kazi Bw. Ibrahim
Mussa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la (ATCL)
wakati alipoizindua rasmi bodi hiyo itakayofanya kazi kwa miaka mitatu
mingine katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Shirika hilo mtaa wa
Ohio jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na
Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akizungumza na wajumbe wa Bodi ya
wakurugenzi ya Shirika la Ndege la ATCL wakati alipokuwa akiizindua
rasmi kwenye ofizi za shirika hilo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano
na Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la ATCL Injini
Emmanuel Koroso pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la ATCL Injini Emmanuel Korosoakizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Shirika la Ndege la ATCL Injini Emmanuel Koroso kushoto na
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Injinia Ladslaus Matindi wakiwa
na wajumbe wa bodi pamoja na watendaji wa shirika hilo katika uzinduzi
huo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la ATCL Injini
Emmanuel Koroso, Mkurugenzi wa Shirika hilo Injini Ladslaus Matindi
pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano
na Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la ATCL Injini
Emmanuel Koroso,Mkurugenzi wa Shirika hilo Injini Ladslaus Matindi
wajumbe wa bodi pamoja na watendaji wa shirika hilo.
No comments:
Post a Comment