Waziri wa Maji Profesa
Makame Mbarawa katikati Mwenye miwani, akizungumza na Madiwani na
Viongozi wa ngazi mbalimbali ofisini kwa Mkuu wa Wilaya (hawapo pichani)
wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji Wilayani humo
kabla ya kuanza ziara kukagua miradi ya Maji.
Waziri wa Maji Makame
Mbarawa na msafara walioongozana wakishuka mlima kutoka mradi wa Maji wa
Luhundwa ambako huko amekagua utekelezaji wa mradi huo, ambao baada ya
kukamilika wananchi wa maeneo hayo watapata huduma ya maji Safi.
Waziri wa Maji Profesa
Makame Mbarawa katikati akisisitiza Jambo baada ya kufika katika moja wa
mitaro ya kupitisha mabomba ya maji kuelekea katika mradi wa maji wa
Luhundwa ambao bado unaendelea na utekelezaji wake ili wananchi
wanaozunguka mradi huo waweze kupata huduma ya maji
Mbunge wa Jimbo la
Mpwapwa George Lubeleje mwenye suti nyeusi katikati akizungumza na
wananchi wananchi waozunguka mradi wa Maji wa Bumila baada ya
kuhakikishiwa huduma ya maji na Waziri wa Maji na mkandarasi tayari
kashapewa fedha kukamilisha mradi huo.
foleni ya madumu na
msimamizi wa kituo Cha maji katika mradi wa Maji wa Bumila ambao
unafanya kazi kwa dharura ili kupunguza makali ya adha ya maji katika
eneo hilo ambapo hata hivyo mkandarasi kashalipwa fedha kukamilisha
mradi huo ili kupanua zaidi huduma ya maji katika eneo hilo.
………………
Na.Alex Sonna,Mpwapwa
Waziri wa Maji Profesa
Makame Mbarawa, amesema wamekusudia kuanzia Sasa kuanzisha
utaratibu wa
kutokutumia wakandarasi au kutoa tenda katika miradi ya maji
inayotekelezwa maeneo mbalimbali hapa nchini na badala yake watatumia
wataalamu wa ndani ya Mamlaka za maji kukamilisha miradi hiyo.
Waziri Mbarawa
ametoa kauli hiyo Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake Wilayani
Mpwapwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji, ambapo amesema wamefikia
hatua hiyo baada ya wakandarasi wengi kuchukua fedha na kutokukamilisha
miradi hiyo, amesema serikali imewekeza fedha nyingi Sana lakini
matokeo yake hayaonakani.
Na kubainisha kuwa
miradi mingi wanapewa wakandarasi ambao hawana uwezo au kupeana tenda
kindugu na kutekeleza miradi chini ya kiwango.
“Serikali za awamu
zote zilizopita ilitenga fedha nyingi Sana kwa ajiri ya miradi ya maji
lakini matokeo yake hayaonekani wote tunajiuliza fedha zinakwenda wapi
wakati maji hayatoki na fedha hazirudishwi na majibu yake kila mtu
anayo”
“Kwahiyo tumeamua
kuja na utaratibu huu wakuto kuwatumia wakandarasi na badala yake
tutatumia wataalamu wa ndani ya Mamlaka zetu za maji na mfano tumefanya
hivyo Mkoa wa Katavi na matokeo tumepata” amesema Waziri Mbarawa.
Katika Ziara hiyo
Wilayani Mpwapwa ametembelea miradi ya maji Luhundwa na Bumila kuona
utekelezaji wake wake na akiwa katika mradi wa Maji wa Bumila, Waziri wa
Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Kata hiyo kuwa hivi karibuni
wataanza kupata huduma ya maji Safi.
Kwani mradi huo
ulikwama kutokana na mkandarasi kutolipwa fedha lakini kwa Sasa
mkandarasi huyo kashalipwa fedha na mradi huo utakamilika ndani ya mda
mfupi na wataanza kupata huduma ya maji.
“Tunajua mkandarasi
wa mradi huu alisimama lakini tumeshamlipa fedha zake na atakuja
kukamilisha mradi huu, pia nishukuru Chama Cha Mapinduzi waliweka pumpu
ya dharura na mkawa mnapata huduma ya maji, Sasa tutapanua zaidi na
kuongeza vituo zaidi ili mpate huduma ya maji kikamilifu naomba muiamini
serikali yenu” amesema.
Awali Mkuu wa Wilaya
ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akitoa taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt Binilith Mahenge, amesema licha ya miradi mingi
kutokukamilika lakini bado huduma ya maji inazidi kuimarika kwani mwaka
2015 ni asilimia 43 tu ndio walikuwa wakipata huduma ya maji na Sasa ni
asilimia 57 kwa miji midogo na Wilaya.
Wakati kwa miji
mikubwa upatikanaji wa maji ilikuwa, ni asilimia 65 na Sasa ni asilimia
82, na wamejipanga angalau kufikia mwaka 2025 kwa miji midogo ifikie
asilimia 80 na miji mikubwa wafikie asilimia 95.
Aliongeza kuwa ” kwa
Wilaya ya Mpwapwa Kuna miradi 10, inayotekelezwa mpaka Sasa, Saba
(7)mipya na mitatu(3) ya ukarabati yote ikiwa na thamani ya shilingi
bilioni 4.17, huku changamoto ikiwa ni fedha kutofika kwa wakati maeneo
husika” amesema DC Shekimweri.
Kutokana na hali ya
kutofika kwa wakati kwa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo Mkuu huyo wa
Wilaya amemuomba Waziri kuhimiza watendaji wa Mamlaka za maji na usafi
wa mazingira Vijijini RUWASA makao makuu kupeleka fedha kwa wakati ili
miradi hiyo ikamilike kwa wakati wananchi waweze kupata huduma ya maji
Safi.
Amesema changamoto
hiyo ya fedha kutofika kwa wakati imekuwa chanzo kikubwa kwa miradi
mingi kutokamilika kwa wakati katika Wilaya hiyo huku wananchi
wakiendelea kupata adha ya maji.
Baadhi ya Wananchi
wa wanaozungua mradi wa Maji wa Bumila wameishukuru serikali kwa kuleta
fedha za mradi huo kwani shida ya maji katika eneo hilo ni kubwa sana
wamesema angalau Sasa adha ya maji itapungua kwa kiasi kikubwa Sana
kwani hiyo ilikuwa kero kubwa Sana kwao
No comments:
Post a Comment