Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt.
Stephen Nindi akifungua kikao cha kikao kazi kuhusu kukamilisha
urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini,
Morogoro, Octoba 2, 2019
Bw. Peter Lorri, Meneja Uhifadhi nchi kavu kutoka Asasi ya kiraia ya The Nature Conservancy (TNC), akieleza ushiriki wao katika uwezeshaji wa upangaji, usimamizi na
utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bw.
Angolile Rayson Afisa Programu kutoka PELUM Tanzania akielezea
ushiriki wao katika Mwongozo wa mpango wa matumizi ya ardhi na namna
walivyoshiriki katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja uandaaji wa
matumizi ya ardhi katika baadhi ya vijiji nchini Tanzania
Bw. Joseph Osena Kaimu Mkurugenzi, mipango ya matumizi ya ardhi,
usimamizi na uratibu akiwapitisha wana kikosi kazi aina 14 za ramani
ambazo zinatakiwa kuandaliwa wakati wa upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya
vijiji ambazo zitaifanya mipango hiyo kuwa ya kisayansi zaidi
Bw.
Paulo Tarimo Mkurugenzi wa Mipango ya ya Matumizi ya ardhi Wizara ya
Kilimo, akichangia jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa
ushirikishaji katika upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bw.
Zakaria Faustin Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la
TNRF akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kukamilisha urejeaji wa
Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Bi.
Albina Burra kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi ya Ardhi (NLUPC) akijibu na kutoa ufafanuzi katika baadhi ya
maswali yaliyoulizwa na wadau katika mjadala wakati wa kukamilisha
urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini
Kikao kazi cha kukamilisha urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji,
usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini, kikiendelea.
Tume
ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na
Mashirika ya TNC pamoja na PELUM-Tanzania imekutana na wadau wa uandaaji
wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini kwa ajili ya kukamilisha
urejeaji wa Mwongozo wa ushirikishaji katika upangaji, usimamizi na
utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini (Guideline for
participatory village land use planning, administration and management
in Tanzania)
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kazi hiyo, M kurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen
Nindi amewataka wadau hao kuhakikisha Mwongozo huo unakuja na majibu ya
kisayansi katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa kuzingatia
ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya tabianchi kwa malengo ya
kuwasaidia wananchi.
No comments:
Post a Comment