Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Balozi wa Uingereza
nchini Tanzania Bi Sarah Cooke mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo
za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo ya
kikazi leo tarehe 2 Octoba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi
wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke katika na ujumbe wake mara
baada ya mzungumzo ya kikazi katika ofisi ndogo za wizara ya Kilimo
Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2 Octoba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari katika
ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2
Octoba 2019. Wengine pichani ni Dkt Maurizio Papaleo kutoka kampuni ya
Oltremare na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya T Masasi Agro Bi Sarah Masasi
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari katika
ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 2
Octoba 2019. Wengine pichani ni Dkt Maurizio Papaleo kutoka kampuni ya
Oltremare na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya T Masasi Agro Bi Sarah Masasi
Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japahet Hasunga ameeleza kuwa mazungumzo hayo
yalijikita zaidi kwenye namna ya kuimarisha zaidi mahusiano na ushirikiano kati
ya nchi hizo mbili ambayo yanaendelea kudumu na kuwa na mafanikio makubwa.
Majadiliano hayo yamehusu pia miradi mbalimbali mahususi ambayo inaweza
kuibuliwa kwa pamoja na kushirikiana wa pamoja ili kufikisha adhma ya serikali
ya awamu ya tano kuwa na maendeleo endelevu kupitia sekta ya viwanda.
Pia majadiliano hayo yalijikita kwenye upanuzi wa kiwanda cha sukari
cha Kilombero Mkoani Morogoro kwani moja ya kampuni za Uingereza ni wawekezaji
katika kiwanda hicho.
Alisema kuwa dhamira ya majadiliano ya kiwanda hicho cha sukari ni
kuona namna ya kuongeza uzalishaji mara dufu ya huu wa sasa.
Kadhalika, katika majadiliano hayo Waziri Hasunga amesema kuwa
wamezungumzia namna ya kuondoa vikwazo vya mashirikiano na vya kufanya biashara
au kufanya uwekezaji nchini na hususani vile ambavyo serikali ya Tanzania
imeviweka katika mkakati wa kuondoa dosari na vipingamizi katika kufanya
biashara nchini vijulikanavyo kama “Blue Print”.
Pia majadiliano kuhusu namna ambavyo serikali imeamua kuja na sera mpya
ya kilimo ya mwaka 2019 na namna ambavyo sheria itatungwa hivyo kupelekea kuwa
na sheria ya kulinda kilimo itakayokuwa na vipaumbele mbalimbali kwa ajili ya
kuimarisha uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Kwa
upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke amesema
kuwa mkutano wake na Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga umekuwa na
mafanikio makubwa ukiwa na mtazamo wa mbali wa kuendeleza sekta ya kilimo.
Cooke
alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta
ya Ardhi kwa kipindi kifupi. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na mpango wa
kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili ASDP II.
Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amekutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza mitambo ya
kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari.
Mhe Hasunga amesema kuwa Mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza
mitambo ya kubangua korosho ya Oltremare ya nchini Italia Ndg Stefano Massari kwa
ushirikianio ya wazawa amemuahidi kuleta mitambo ya kisasa ili kujenga kiwanda
kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kubangua Tani 30,000 kwa mwaka.
Amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utapelekea kufikia lengo la
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho zote
zinazozalishwa zinabanguliwa hapa hapa nchini.
“Na tukifanya hivyo tayari tutakuwa tumefanikiwa kuitangaza nchi yetu
vizuri kwani tutakuwa tunauza korosho ambazo zimebanguliwa hapa hapa nchini”
MWISHO
No comments:
Post a Comment