Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na
wananchi wa Baleni wilayani Mafia mkoa wa Pwani alipokwenda kusikiliza
kero za ardhi katika eneo hilo akiwa katika ziara yake ya siku mbili
katika wilaya hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia
kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
Mwananchi
Hassan Omar maarufu mzee wa Lumbesa mkazi wa Dagoni Mafia akimuonesha
nyaraka Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula kuhusiana na mgogoro wa ardhi wakati Dkt Mabula alipofanya ziara
wilaya ya Mafia kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia
kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya ardhi jana.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akikagua Majalada ya Ardhi katika ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mafia jana wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua masijala ya
ardhi jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaib Nnenduma na Kulia
ni Afisa Ardhi Chuchu Ochere.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia baadhi ya Nyaraka za umiliki wa ardhi kutoka kwa Hassan Mohamed (Kushoto) na Mwanangano Mohamed wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya ya Mafia jana (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
No comments:
Post a Comment